Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:44

Wanajeshi wa Somalia waliokwenda kwenye mafunzo Eritrea warejea


wanajeshi wa somalia
wanajeshi wa somalia

Amesema Kundi la kwanza la wanajeshi elfu tano wa Somalia wamerejea nyumbani katika Pembe ya Afrika wanatarajiwa kupelekwa kukabiliana na uasi wa wanamgambo wa kiislamu.

Kurejea kwao kumemaliza wasiwasi miongoni mwa familia ambazo zilihofia pengine walikuwa wameandikishwa kwa udanganyifu na kushikiliwa mateka.

Waziri wa ulinzi wa somalia Abdulkadir Mohamed Nur ameelezea kuwa ni habari njema, kwamba wamerejeshwa nyumbani.

Uvumi ulizuka katika taifa hilo lenye watu milioni 17 kwamba wanajeshi wanaweza kuwa wamepelekwa katika mkoa wa Tigray uliokumbwa na vita.

Anasema “ leo nataka kushirikiana pamoja nanyi habari njema ambayo ni muhimu kwa watu wa somalia na katika mapambano dhidi ya al- shabaab . kundi la kwanza la wanajeshi wa somalia lililopatiwa mafunzo Eritrea limerejea nchini na waliobaki watarudi katika siku zijazo. Wanajeshi waliopatiwa mafunzo watakuwa sehemu ya mpambano na al- shabaab.

XS
SM
MD
LG