Wanajeshi wa Eritrea walipigana pamoja na wanajeshi wa Ethiopia na wanamgambo washirika katika mzozo wa miaka miwili uliowahusisha serikali ya Ethiopia dhidi ya vikosi vya waasi katika eneo la kaskazini la Tigray.
Mwezi Novemba, hata hivyo, serikali ya Ethiopia na vikosi vya Tigray vilitia saini makubaliano ya kumaliza uhasama. Mkataba huo uliamuru kuondolewa kwa vikosi vyote vya kigeni kutoka Tigray.
“Kuhusiana na Waeritrea tunaelewa kuwa wamerudi mpakani na wametakiwa kuondoka,” Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, alisema katika mkutano na waandishi wa habari alipoutembelea mji mkuu wa Kenya Nairobi.