Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 27, 2025 Local time: 19:56

Henry Kissinger- mwanadiplomasia wa Marekani aliyekuwa mtata na atakaye enziwa afariki akiwa na umri wa miaka 100


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wa zamani Henry Kissinger, Agosti 10, 1976 akiwa Ufaransa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wa zamani Henry Kissinger, Agosti 10, 1976 akiwa Ufaransa.

Henry Kissinger, Mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa na Waziri wa Mambo ya Nje ambaye ushawishi wake kimataifa ulibakia kwa kipindi kirefu baada ya kuondoka madarakani akiwa chini ya Rais wa zamani Richard Nixon, amefariki akiwa na umri wa miaka 100, nyumbani kwake huko Connecticut.

Kifo chake kilitangazwa na kampuni yake ya ushauri na hakuna sababu iliyotolewa. Mwandishi mwanadamizi wa kidiplomasia Cindy Saine anaripoti kuhusu maisha na urithi aliouacha kiongozi wa kitaifa wa Marekani aliyekuwa na utata na mwenye kuenziwa.

Henry Kissinger alizaliwa na Heinz Afred Kissinger mwezi Mei 27, 1923, huko Fuerth, Ujerumani.

Yeye na familia yake, ambao ni Wayahudi, walikimbilia Marekani mwaka 1938 waliwakimbia Wanazi. Alijiunga na jeshi la Marekani wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, na baadae kusoma Chuo Kikuu cha Havard na kujiunga na kitivo hicho.

Alipoingia madarakani mwaka 1969, wakati huo Rais Richard Nixon alimchagua kuwa mshauri wake wa usalama wa taifa.

(FILES) Rais wa zamani wa Marekani Richard Nixon (Kushoto) akiwa na Henry Kissinger, Waziri wa Mambo ya Nje, Septemba 1973, Washington.
(FILES) Rais wa zamani wa Marekani Richard Nixon (Kushoto) akiwa na Henry Kissinger, Waziri wa Mambo ya Nje, Septemba 1973, Washington.

Baadaye pia aliteuliwa waziri wa mambo ya nje, na kuwa mtu wa kwanza kushikilia nafasi zote mbili kwa wakati mmoja.

Kissinger aliweka aina yake ya “uhalisia wa kisiasa” msingi wa sera ya mambo ya nje na kile alichosema ni utekelezaji, kuliko kwa wakati huo maamuzi ya kimaadili.

Aaron David Miller alitumikia uongozi kadhaa wa Warepublikan na Wademokratiki, lakini siyo Kissinger.

FILE - Makamu Rais wa Kituo cha Wilson Aaron David Miller, kushoto, akizungumza na Waziri wa Ulinzi wa Israeli Moshe Ya'alon katika kituo cha Wilson Center, Washington, Jumatatu, Machi 14, 2016.
FILE - Makamu Rais wa Kituo cha Wilson Aaron David Miller, kushoto, akizungumza na Waziri wa Ulinzi wa Israeli Moshe Ya'alon katika kituo cha Wilson Center, Washington, Jumatatu, Machi 14, 2016.

Aaron David Miller wa Taasisi ya Carnegie Endowment for International Peace anaeleza:

“Wakosoaji wake watatoa hoja kuwa alikuwa mkatili na asiyejali hali ya wengine. Wengine wanadai, na hilo linaweza kuwa kweli kwa idadi yoyote ya viongozi wa Marekani, kuwa inatakiwa achukuliwe kama mhalifu wa kivita, kuhusiana na Cambodia, Cambodia na Laos … sera zake kwa Bangladesh mwanzoni mwa miaka ya 70. Lakini ukweli ni kuwa aliathiri diplomasia katika njia kadhaa ambazo zilikuwa siyo za kawaida.”

Kissinger hakuweka wazi kwa Bunge la Marekani mashambulizi ya bomu kwa njia ya anga yaliyofanywa na Marekani huko Cambodia na Laos, ambayo yalichochea zaidi Vita ya Vietnam.

Lakini ilikuwa Kissinger pia ambaye alikutana mara nyingi na Le Duc Tho wa Vietnam Kaskazini kujadili kumaliza vita hivyo, na kwamba wote wawili walipewa Tuzo ya Nobel ya Amani mwaka 1973. Le Duc Tho aliikataa.

Kissinger alijihusisha na China mwaka 1972, akifanya maandalizi ya ziara ya Rais wa wakati huo Nixon katika nchi ya Kikomunisti kukutana na Mwenyekiti Mao Zedong, ziara ya kwanza ya rais wa Marekani.

(FILES) Hayati Henry Kissinger (Kulia) akikutana na Mwenyekiti Mao Zedong, 24 Novemba,1973, Beijing.
(FILES) Hayati Henry Kissinger (Kulia) akikutana na Mwenyekiti Mao Zedong, 24 Novemba,1973, Beijing.

Hili lilihesabiwa kama ni moja ya ushindi kadhaa mkubwa wa Kissinger, lakini Jarrod Hayes wa Chuo Kikuu cha Massachusetts, Lowell ana maoni tofauti, akisema Kissinger alikuwa mtaalam wa kutengeneza sera.

Anaendelea kusema : “Alibadilisha ufahamu wa diplomasia kupitia mwenendo wake wa ziara za kidiplomasia, alifanya ionekane kuwa ni ya umuhimu wa juu, na kuifanya kuwa ya kuvutia.

Aliifanya hivyo, unajua, kuwa ya kupendeza, kama utapendelea hivyo. Na hivyo basi, hilo linamfanya awe na chapa ya kipekee ya sera ya mambo ya nje. Lakini ukiondoa hiyo chapa, na iwapo utakwenda ndani zaidi, hiyo siyo sera ya nje ijulikanayo ambayo imeisaidia Marekani kufanya vizuri.”

Kissinger alimshauri kila rais wa Marekani kuanzia Nixon, hadi Rais Joe Biden, ambaye hakumkaribisha katika ofisi yake ya Oval, huko White House.

Rais wa Marekani Joe Biden Picha na RONEN ZVULUN / POOL / AFP.
Rais wa Marekani Joe Biden Picha na RONEN ZVULUN / POOL / AFP.

Ushawishi wake wa muda mrefu hauna upinzani, profesa wa historia Michael Kimmage anasema.

Lakini haamini kuwa falsafa ya Kissinger ya “Realpolitik”, au sera halisi ya kimaslahi iliyoepuka maadili, imeendelea kuwa ni sera ya mambo ya nje ya Marekani.

Michael Kimmage, wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Marekani ameeleza:

Ameongeza kuwa: “Nafikiri kuwa yeye mwenyewe anafahamu vilivyo kuwa ukakasi unaogubika sera ya mambo ya nje ya Marekani ni kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni uliberali wa kimataifa, au “Wilsonianism” inayofungamana na Rais Woodrow Wilson, ambaye aliunda Umoja wa Mataifa na kupigana Vita vya Kwanza vya Dunia chini ya tamko, ‘iweke dunia salama kwa ajili ya demokrasia’. Hii ndio hakika utamaduni uliobobea wa sera ya kigeni ya Marekani, na Kissinger ni kama mpinzani wa hilo. Na kwa hisia hiyo, sidhani, kwa namna yoyote ile, amefuzu kwa hoja hiyo.”

FILE Woodrow Wilson
FILE Woodrow Wilson

Kissinger alianzisha utata zaidi mwaka 2022, alipojitokeza na kusema Ukraine ni lazima iwe tayari kuachia baadhi ya ardhi yake kumaliza uvamizi wa Russia.

Ni ripoti ya Cindy Saine, VOA News.

Forum

XS
SM
MD
LG