Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:53

Mandela azikwa


Familia na wageni mashuhuri wakati wa mazishi ya Nelson Mandela, Desemba 15, 2013
Familia na wageni mashuhuri wakati wa mazishi ya Nelson Mandela, Desemba 15, 2013
Wananchi wa Afrika Kusini wamemuaga kwa mara ya mwisho Nelson Mandela ambaye amezikwa katika kijiji alichokulia cha Qunu leo Jumapili.

Watu wapatao 4,500 kutoka familia yake na wageni mashuhuri walikusanyika katika kijiji hicho kidogo kuhudhuria ibada ya mwisho na mazishi ya rais huyo wa zamani, kukiwa na muziki na hotuba za kumsifu marehemu Mandela.

Baadaye wageni wachache tu waliungana pamoja na familia yake kwenye kaburi ambako mwili wa Mandela ulizikwa huku mizinga 21 ikifyatuliwa na helikopta za kijeshi na ndege zikipeperusha bendera ya Afrika Kusini na kupaa juu ya kaburi lake wakati wa mazishi hayo.

Sherehe za leo Jumapili zimehitimisha siku 10 za maombolezi ya bw. Mandela, rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini na shujaa wa ukombozi aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Akizungumza katika mazishi hayo rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alimweleza Mandela kama, chanzo cha hekima, nguzo imara na matumaini kwa wote wanaopigana kuishi katika dunia yenye haki na usawa.
XS
SM
MD
LG