Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 19:13

Rais Biden na mkewe Jill wahudhuria ibada ya mazishi ya Malkia Elizabeth II

Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakiwa katika ibada ya mazishi ya Malkia Elizabeth II.
Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakiwa katika ibada ya mazishi ya Malkia Elizabeth II.

Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill Biden walikuwa miongoni mwa viongozi wa dunia waliohudhuria ibada ya mazishi ya Malkia Elizabeth.

Pia waliungana pamoja na familia ya ufalme na kikundi kidogo cha waalikwa katika kanisa la Westminster Abbey, wakienzi miaka 70 ya kutumikia taifa kama malkia aliyetawala kwa kipindi kirefu Uingereza.

Rais Biden aliwasili jioni Jumamosi kwa ajili ya shughuli hii na amekuwa kimya katika mji mkuu wa Uingereza, hakufanya mikutano yoyote ya kidiplomasia na wakiongelea suala la kifo cha malkia kilichotokea Septemba 8 akiwa na umri wa miaka 96.

Maafisa wa White House wameiambia VOA kabla ya maziko kuwa uhusiano thabiti kati Washington na London utaendelea baada ya mabadiliko ya uongozi ya hivi karibuni – ikiwemo Mfalme mpya, Charles III, na waziri mkuu aliyepitishwa hivi karibuni, Liz Truss. Biden atakutana na Truss Jumatano huko New York, pembeni ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Mfalme wa Uingereza Charles III alipokutana kwa mara ya kwanza na Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss katika Kasri ya Buckingham, London, Sept. 9, 2022 kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II.
Mfalme wa Uingereza Charles III alipokutana kwa mara ya kwanza na Waziri Mkuu wa Uingereza Liz Truss katika Kasri ya Buckingham, London, Sept. 9, 2022 kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II.

“Tunaimani kuwa kuchukua uongozi kwa Mfalme Charles na Waziri Mkuu Truss uhusiano huu maalum kati ya Marekani na Uingereza utadumu, hatuna wasiwasi juu ya hilo kabisa,” mkurugenzi wa Baraza la Usalama wa Taifa wa mawasiliano ya kimkakati John Kirby ameiambia VOA.

Siku ya Jumapili, Biden na mke wake walitoa heshima zao za mwisho wakati mwili wa malkia ukiwa umewekwa kitaifa katika Ukumbi Westminster, wakati maelfu ya watu wakiwa wamejipanga kwa saa kadhaa kupita kutoa heshima katika jeneza la malkia lililofunikwa, ambalo lina Nembo ya Himaya ya Ufalme , yenye thamani na inayotambulika iliyofunikwa na almasi ya Afrika inayomeremeta, yenye kareti 530 aliyopewa Malkia na koloni la Afrika Kusini mwaka 1907.

Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakitoa heshima zao kwa mwili wa Malkia Elizabeth II katika Ukumbi wa Westminster huko katika kasri ya Westminster, London, Sept. 18, 2022.
Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakitoa heshima zao kwa mwili wa Malkia Elizabeth II katika Ukumbi wa Westminster huko katika kasri ya Westminster, London, Sept. 18, 2022.

Siku ya Jumapili, Biden alisaini kitabu cha maombolezo, na rais alimpongeza malkia kwa kuacha athari ya utumishi wake usiokuwa na ubinafsi.

XS
SM
MD
LG