Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:00

Maelfu wasongamana wakitaka kuliona jeneza la Malkia Elizabeth


Maelfu ya raia wa Uingereza wasubiri kuona jeneza lililobeba mwili wa Malkia Elizabeth.
Maelfu ya raia wa Uingereza wasubiri kuona jeneza lililobeba mwili wa Malkia Elizabeth.

Mamia ya waombolezaji Jumanne walipanga foleni nje ya ikulu ya Buckingham na katika mitaa ya mji wa London, nchini Uingereza, wakati msafara wa magari uliokuwa ukiandamana na lile lililobeba jeneza la Malkia Elizabeth wa pili, ukielekea kwenye makao ya kifalme.

Mamia ya waombolezaji jana Jumanne walipanga foleni nje ya ikulu ya Buckingham na katika mitaa ya mji wa London, nchini Uingereza, wakati msafara wa magari uliokuwa ukiandamana na lile lililobeba jeneza la Malkia Elizabeth wa pili, ukielekea kwenye makao ya kifalme.

Ndege ya kijeshi ya C-17 iliyobeba jeneza hilo iliwasili mjini London kutoka mjini Edinburgh, Scotland, mapema Jumanne, ikisindikizwa na binti pekee wa malkia, Princess Anne, na mume wa Anne, Sir Timothy Laurence.

Jeneza hilo, lililopambwa kifalme, litasalia usiku kucha katika Chumba kiitwacho Bow room.

Leo Jumatano, jeneza hilo litahamishwa kwa msafara utakaoongozwa na Mfalme Charles III hadi Ukumbi wa Westminster, wa karne ya 11, ambapo mwili wa malkia utalazwa kwa siku nne.

Ukumbi huo utakuwa wazi kwa saa 23 kwa siku, kwa wageni na utalindwa na askari wa kifalme. Maelfu ya watu wanatarajiwa kusafiri hadi Westminster kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Elizabeth alifariki Septemba 8 katika Kasri la Balmoral, katika Milima ya Scotland, mahali alipopapenda sana, na ambapo Charles alikua mfalme. Siku ya Jumanne, Charles alitembelea Ireland Kaskazini katika safari yake ya kwanza huko kama mfalme. Aliandamana na mke wake, Camilla.

Malkia Elizabeth atazikwa tarehe 19 mwezi huu.

XS
SM
MD
LG