Prince Charles aliweka shada la maua siku ya Jumatano katika kumbukumbu ya mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda wakati wa ziara yake ya kwanza iliyofanywa na familia ya kifalme ya uingereza nchini Rwanda.
The Prince of Wales na mkewe Camila, walikaa kimya wakati wa kutoa heshima katika kumbukumbu ya mauaji ya kimbari mjini Kigali, mahala pa mwisho walipolazwa zaidi ya waathirika 250,000 wa mauaji hayo karibu miongo mitatu iliyopita.
Wanandoa hao wa kifalme, walitia saini kitabu cha kumbukumbu kilichoandamana na shada la maua meupe.
Pia walizungumza na manusura wa mauaji ya kimbari, ambapo takribani watu laki nane hasa Watutsi, waliuawa na vikosi vya wahutu wenye msimamo mkali, kati ya April na Julai mwaka 1994.
Mafuvu, vipande vya mifupa, na vipande vya nguo, kumbu-kumbu hii ni ushahidi wa maovu ya mauaji ya kimbari, yaliyowekwa kwenye kituo cha utamaduni cha wageni mashuhuri wanaotembelea Rwanda.
Charles na Camila, pia walitembelea jumba la kumbukumbu ambapo walitazama picha za waathirika na mali zao, na walisikia maelezo ya binafsi ya mauaji hayo.
Wanandoa hao wa kifalme waliwasili Jumanne jioni nchini Rwanda, ambapo Prince of Wales, anamwakilisha mama yake, Queen Elizabeth wa pili, katika mkutano wa kilele wa jumuiya ya madola wiki hii.
Viongozi wa mataifa mengi katika Jumuiya ya Madola, wanatarajiwa mjini Kigali katika siku zijazo kwenye mkutano wa wanachama 54 wa klabu hiyo, ya koloni la zamani la uingereza.