Mwandishi wa voa ameripoti kuwa Ahmed Kathrada alikuwa mtoto alipoanzisha harakati za kutaka haki sawa katika nchi aliyozaliwa ya Afrika Kusini na kuwa ni harakati zake za kudumu.
Alikuwa na mtoto wa kiume wa miaka 12 pale alipojiunga na Young Communist League katika taifa hilo, ambayo ilikuwa ikipinga ubaguzi wa serikali.
Alipokuwa na umri wa miaka 17, alikamatwa kwa kuvunja sheria ambazo zilikuwa za kibaguzi dhidi ya wananchi wa afrika kusini wenye asili ya kihindi.
Harakati zake dhidi ya ubaguzi
Mwaka 1964, yeye na wenzake sita walisimamishwa kizimbani pamoja na watetezi wakuu wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela na Walter Sisulu pale jaji alipowahukumua kifungo cha maisha jela kwa juhudi zao za kuvuruga utawala wa weupe walio wachache.
Kathrada alikaa gerezani kwa takriban miaka 26, miaka 18 kati ya hiyo alifungwa pamoja na mandela ambaye baadaye akawa rais wa kwanza mweusi mwaka 1994 na kujulikana kama baba wa taifa.
Katika mazishi ya mandela mwaka 2013, Kathrada alilia sana akikumbuka uhusiano wake na mandela.
"Walter Sisulu alipofariki nilimpoteza baba. Na hivi sasa nimempoteza kaka. Maisha yangu ni matupu na sijui nimgeukie nani," alisema.
Kifo cha Kathrada katika umri wa miaka 87 pia ni kama suala la kifamilia nchini Afrika Kusini. Muda mfupi baada ya kifo chake kutangazwa Jumanne, Rais Jacob Zuma alitangaza mazishi rasmi na kuamuru bendera zipeperushwe nusu mlingoti kote nchini humo, kwa mtu ambaye taifa lote linamjua kama mjomba Kathy.
Taasisi ya Nelson Mandela
Mtendaji mkuu wa taasisi ya Nelson Mandela Sello Hatang amesema kathrada alikuwa zaidi ya rafiki kwa Mandela, ambaye Hatanga anamtaja kwa jina lake la asili la Madiba.
"Madiba alisema alijiweka na marafiki ambao wanaweza kumueleza pale anapokosea. Na alimuona bwana Kathrada kama mmoja wa marafiki hao, ambaye aliweza kumwambia kuwa anavyofanya ni makosa," amesema Hatanga.
Mandela alikuwa karibu sana na kathrada wakati wa urais wake, na kumfanya mshauri wake wa juu wa kisiasa.
Katika miaka yake ya mwishoni, Kathrada aliendelea kuwa sauti ya uadilifu, na kuelekeza baadhi ya maoni yake kwa Zuma, ambaye alikumbwa na kadhia kadhaa za rushwa.
Barua ya wazi kwa Zuma
Mwaka jana katika barua ya wazi, alimtaka zuma ajiuzulu na kusema, komrade rais, hudhani kuwa kuendelea kuwepo kwako madarakani kama rais kutaimarisha mgogoro katika serikali humu nchini.
Hatanga pia amewasihi wananchi wa Afrika Kusini kusherehekea maisha ya Kathrada kwa kujaribu kukumbuka misingi yake.
Kathrada atazikwa mjini Johannesburg Jumatano kwa taratibu za dini ya Kiislamu.