Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:32

Kanisa Katoliki latishia kujiitoa katika upatanishi DRC


Kanisa Katoliki mjini Kinshasa
Kanisa Katoliki mjini Kinshasa

Ghasia zimetokea katika baadhi ya maeneo nje ya mji mkuu wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo Jumanne, baada ya maaskofu wa Kanisa Katoliki kujitoa katika nafasi yao ya usuluhishi.

Maaskofu hao walikuwa wanafanya juhudi kuzikutanisha pande mbili za serikali na upinzani katika mazungumzo yaliyokuwa yamekusudia kutafuta ufumbuzi wa kucheleweshwa kwa uchaguzi mwaka huu.

Waandamanaji, wengine wakichoma matairi katika makutano ya barabara, waliandamana katika njia kadhaa huko Kinshasa. Wakati mmoja, polisi walipiga mabomu ya machozi ili kukitawanya kikundi kidogo cha vijana.

Maduka mengi yalikuwa yamefungwa na baadhi ya shule ziliwataka wazazi kuja kuwachukua watoto wao, Shirika la habari la Reuters limeripoti.

Kipindi cha utawala cha Rais Joseph Kabila kilifikia kikomo Disemba lakini uchaguzi ulikuwa haukufanyika katika kile serikali ilichosema ni matatizo ya bajeti, na kusababisha madamano yenye fujo karibuni na mwisho wa mwaka jana ambapo majeshi ya usalama yaliwaua sio chini ya watu 40.

Mkutano wa maaskofu wa Kongo (CENCO) walisaidia kufanya mazungumzo kufikia makubaliano ya Disemba 31 yaliyokuwa na kusudio la kuepusha mgogoro wa kisiasa kwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika mwaka huu kumchagua atayechukua nafasi ya Kabila.

Januari, maaskofu walitahadharisha kuwa makubaliano hayo yanaweza kupata mashaka iwapo wanasiasa hawatofanya haraka kufikia mwafaka na kutekeleza makubaliano hayo.

Maaskofu walijiondosha Jumanne baada ya utekelezaji wa makubaliano hayo kukwama, na kuwepo uwezekano wa kuzuka upya uvunjifu wa amani katika nchi ambayo imekumbwa na mfululizo wa vita na uasi.

“Tunafikiri kuwa hakuna kitu tunachoweza kufanya, “Donatien Nshole, katibu mkuu wa CENCO, ameiambia Reuters.

“Tumetoa muda wetu wote na nguvu zetu zote na hivi sasa kazi yao ya uchungaji imeathirika.”

XS
SM
MD
LG