Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 04:44

Hatimaye Baseball yaiunganisha Washington iliyogawanyika kisiasa


Uwanja wa Nationals Park Washington, ambako mashindano ya ligi ya michuano ya baseball inafanyika.
Uwanja wa Nationals Park Washington, ambako mashindano ya ligi ya michuano ya baseball inafanyika.

Michezo inaweza kuwa ni daraja la kuunganisha pande hasimu kati ya mafahali wa muda mrefu katika diplomasia za kimataifa.

Mfano kama huo unaowaunganisha watu unaweza kupatikana katika maeneo ya kazi, angalau kwa kipindi kifupi, katika mji wa makao makuu ya Marekani ambao umegawanyika kisiasa.

Maelfu ya mashabiki wa timu ya Washington Nationals kutoka tabaka mbalimbali za kisiasa walikuja kushuhudia tafrija zilizokuwa zinaendelea katika uwanja wa nyumbani wiki hii, wakati timu yao ikishinda michezo miwili ya kwanza bora kati ya ligi ya baseball ya michuano saba itayofululiza dhidi ya timu ya Houston Astros huko Texas.

“Nafikiri inatupa nafasi ya kufanya kitu kikubwa zaidi, na kitu kikubwa zaidi kukitegemea, na inatupa sote kitu fulani cha kuwa ni sehemu ya hilo, na kufuatilia, na kukipenda sote kwa pamoja mara moja,” shabiki wa Nationals Sharon Schwei ameiambia Sauti ya Amerika (VOA).

Kushiriki kwa timu ya Nationals kwa mara ya kwanza katika michuano hii ya Ligi ya michuano ya baseball ni mandhari ya kufurahisha katika jiji ambalo mara nyingi limegubikwa na uhasimu baina ya vyama vya siasa.

Mvutano wa kisiasa katika mji wa makao makuu ya Marekani wakati wote hupamba moto ambapo Wademokrat wakiwa wanaendesha uchunguzi unaotaka kumuondosha Rais Donald Trump madarakani, na Warepublikan wengi wanalalamika kuwa ni mchezo mchafu unaoendelea.

Katikati ya uadui wa kisiasa, mashabiki wa timu ya Nationals wanaona ziko sababu za kutosha kuwa pamoja kufurahia ushindi huu, bila ya kujali nani ni mfuasi wa chama gani.

“Nafikiri inatuleta sote pamoja, kila mmoja akiwa na maoni tofuati ya kisiasa, na maoni tofauti juu ya maisha,” shabiki wa Nationals Ali ameiambia VOA.

Baadhi ya mashabiki wanahisi kuwa umoja ulioletwa na timu ya Nationals utapunguza mvutano wa kisiasa wa kichama katika jiji la Washington.

XS
SM
MD
LG