Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:17

Hamdok asema jaribio la kutaka kumuua ni motisha ya kuleta mabadiliko Sudan


Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdo
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdo

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, amenusurika kifo baada ya shambulizi dhidi ya msafara wake Jumatatu katika mji mkuu wa Khartoum kufeli.

Hamdok, aliyeteuliwa mwaka uliopita kuongoza serikali ya mpito baada ya kupinduliwa kwa rais wa mda mrefu Omar Al-Bashir, amepelekwa katika sehemu salama.

Katika ujumbe wa Tweeter Hamdok aliwahakikishia wananchi wa Sudan kwamba yuko salama na kusema kilichotokea ni jambo linalowatia motisha kuleta mabadiliko Sudan.

Televisheni ya taifa ya Sudan imeripoti tukio hilo huku video zikionyesha magari yaliyokuwa kwenye msafara wa Hamdok, yaliyoharibiwa, zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema shambulizi hilo limetokea karibu na daraja la Kober, upande wa Kaskazini, ilipo ofisi ya Hamdok. Inaripotiwa kuwa msafara wa waziri mkuu, umeshambuliwa kutoka juu.

Baadhi ya wakazi wa mji mkuu wa Sudan wa Khartoum wamekuwa wakisherekea kwa kuimba kutokana na habari kwamba Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amenusurika kutokana na jaribio la mauwaji mapema leo.

Msafara wa Hambdok ulishambuliwa kwa bomu kwenye mji mkuu wa Khartoum alipokua anaelekea kazini leo asubuhi. Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika.

Hamdok aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa taifa hilo mwezi Agosti mwaka 2019 kuongoza utawala wa mpito baada ya kuondolewa madarakani kwa Omar al Bashir kufuatia miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya utawala wake.

Shambulio limetokea wakati serikali ya Hamdok ikijaribu kutanzua mzozo mubwa wa kiuchumi nchini humo.

Baada ya Bashir kuondolewa madarakani anazuiliwa kwenye jela maarufu ya Kober ambako wapinzani wake wengi walizuiliwa awali.

Mwezi uliopita serikali ya Sudan ilisema kuwa ingemwasilisha Bashir mbele ya mahakama ya kimataiafa ya jinai ya ICC kwa tuhuma za uhalifu wa kivita pamoja na mauwaji ya halaiki.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG