Kikundi hicho kimetangaza kuwa kitapinga mpango wowote utakao pendekezwa ambao utapunguza haki za Wapalestina.
Akizungumza na shirika la habari la Reuters Meshaal anasema wameanza juhudi za kuhakikisha mpango huo hautatekelezwa wala kufanikiwa.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameusifu mpango huo kama nafasi nzuri ya kupatikana amani alipokutana na Rais Vladimir Putin mjini Moscow. Putin hakuutaja mpango huo wakati viongozi hao walipokutana.
Netanyahu alifunguliwa rasmi mashtaka mahakamani Israel hapo Jumanne wakati mpango huo ukitangazwa huku akikabiliwa na ushindani mkubwa katika uchaguzi ujao wa mwezi Machi akiwa na matumaini mpango huo utaimarisha nafasi yake ya kushinda uchaguzi huo.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.