Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 21:49

Hali ya wakimbizi barani Afrika


 Kambi ya Wakimbizi waliokimbia vita Sudan ya Ourang , Adre Decemba 7, 2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP.
Kambi ya Wakimbizi waliokimbia vita Sudan ya Ourang , Adre Decemba 7, 2023. Picha na Denis Sassou Gueipeur / AFP.

Mashirika ya misaada yanasema migogoro ya Sudan, Somalia, Sahel, na maeneo mengine yanapokea ufadhili mdogo, kuliko unaohitajika kushughulikia changamoto zinazowakabili.

Mapema mwezi huu, mkuu wa baraza la wakimbizi la Norway (NRC) amesema kutelekezwa kabisa kwa watu waliokimbia makazi yao limekuwa ni jambo la kawaida.

Umoja wa Mataifa unasema takriban watu milioni 120 walihamishwa kwa lazima mwaka 2023, na kufanya kuwa mwaka wa 12 mfululizo ambapo idadi hiyo imeongezeka.

Mwezi huu Jan Egeland, mkuu wa baraza la wakimbizi la Norway au NRC, amesema kupuuzwa kabisa kwa watu waliohamishwa imekuwa kawaida mpya.

NRC inasema Burkina Faso ina zaidi ya watu milioni mbili waliokimbia makazi yao, na kuifanya kuwa moja ya janga la waliohamishwa lililopuuzwa zaidi duniani.

Fatoumata Pessako, mama wa watoto tisa alikimbia kaskazini mwa Burkina Faso miaka mitano iliyopita na anasema msaada umepungua toka wakati huo.

“Hapo awali, tulisajiliwa na serikali, lakini hatukupata msaada wowote kutoka kwao. Mashirika machache ya kutoa misaada yalitusaidia, lakini msaada wao umepungua sana, na sasa wanakuja kwa nadra,” anasema.

Afisa mmoja mwandamizi wa misaada ya kibinadamu ameiambia VOA kwamba idadi kubwa ya migogoro ya kimataifa inadhoofisha utashi wa kisiasa wa kuyatatua.

“Ingawa ni kweli kwamba ufadhili wa kazi za kibinadamu umeongezeka kwa miaka mingi, ni kweli pia idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu imeongezeka kwa kasi zaidi kuliko uwezo wa sekta wa kuwafikia,” alisema Ciran Donnely.

Hali kama za Pessako zinatia wasiwasi anasema Ciaran Donnelly.

“Hawa watu wamekwama. Wamehifadhiwa vizuri, neno ambalo ni baya kutumia wakati wa kuzungumza kuhusu watu. Hilo ni eneo moja ambalo hatuoni uwekezaji wowote wa kweli katika kutafuta suluhu.”

Will Carter ni mkurugenzi wa baraza la wakimbizi la Norway kwa Sudan.

“Sijawahi kuona mazingira duni ya ufadhili kama haya, ambayo yamesababisha huduma mbaya kwa watu wenye njaa. Sijawahi kuona kiwango kama hicho cha kidiplomasia na kwa kiwango fulani kupuuzwa na vyombo vya habari juu ya migogoro ya kutisha,” alisema Carter.

Pessako anasema anaelewa matatizo ya ufadhili na anaombea mzozo huo umalizike.

“Jumuiya ya kimataifa ina wasiwasi kuhusu hali yetu, na wakati wa mzozo wa Burkina Faso unaendelea, ninaelewa kuwa si rahisi kwao pia. Naomba mgogoro umalizike ili nirudi kijijini kwangu,” anasema.

Kama mamilioni ya wakimbizi wengine, anachotaka kufanya ni kurudi nyumbani.

Forum

XS
SM
MD
LG