Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:35

Majeshi ya Israel yadaiwa kukiuka kanuni za msingi za vita


Wapalestina wakiwa wamepanda mkokoteni katika eneo lawatu waliopoteza makazi huko Rafah Juni 19, 2024, Picha na Bashar TALEB / AFP
Wapalestina wakiwa wamepanda mkokoteni katika eneo lawatu waliopoteza makazi huko Rafah Juni 19, 2024, Picha na Bashar TALEB / AFP

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa mashambulizi ya anga ya Gaza huenda kwa mara nyingi yalikiuka sheria za kimsingi za vita.

Ripoti iliyotolewa Jumatano ilichunguza msahambilizi sita ya anga yaliofanywa na jeshi la Israel kati ya Oktoba na Desemba mwaka jana wakati wa wiki za kwanza za vita vya Gaza.

Zaidi ya watu 200 walidhibitishwa kufa na ofisi ya haki za binadamu kutokana na mashambulizi hayo yaliolenga makazi ya watu, shule, soko, pamoja na kambi ya wakimbizi.

Kamishna wa baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Turk amesema kuwa inaoneka kuwa Israel haikufanya juhudi zozote za kutofautisha raia wa kipalestina na wapiganaji wa Hamas, wakati wa kurusha mabomu huko Gaza.

“Maisha ya watu pamoja na miuondomusingi imelindwa” chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu,” amesema Turk.

Ameongeza kusema kuwa sheria ni dhahiri kwamba pande zinazopigana zinahitaji kuweka kipaumbelea kwenye kulinda maisha ya watu. Ripoti hiyo imesema kuwa mashambulizi 6 yaliochunguzwa yanashukiwa kutumia mabomu mazito ya kilo kati ya kilo 113 na 907.

Ripoti hiyo imeongeza kusema kuwa mashambulizi ya makombora ya makundi yenye silaha ya Palestina dhidi ya Israel, hayaendani na sheria kimataifa za kibinadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG