Wakati huo huo, Marekani inaendelea kufanya tathmini kuhusu shehena moja ya mabomu kwa Israel kutokana na wasiwasi juu ya matumizi ya mabomu hayo katika eneo la Rafah lenye watu wengi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Jumanne amesema kwamba maafisa wanatafuta njia ya kidiplomasia kumaliza mapigano kwenye mpaka wa kaskazani wa Israel na Lebanon ili raia warejee makwao kwa usalama.
“Hezbollah imehusisha mashambulizi inayoyafanya dhidi ya Israel na yale yanayofanywa na Israel huko Gaza,” Blinken aliwambia waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari pamoja na katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg.
“Tukipata sitisho la mapigano Gaza, nadhani hali hiyo inaweza kupelekea kupatikana kwa suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo huko Kaskazini.”
Huko Beirut, mjumbe maalum wa Marekani Amos Hochstein amehimiza kusitishwa kwa mzozo kati ya Israel na Hezbollah.
Forum