Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:59

Marekani inasema hatua ya Netanyahu kulivunja baraza lake la vita ni maamuzi ya ndani


Mratibu wa mawasiliano wa Baraza la usalama wa taifa wa Marekani, John Kirby
Mratibu wa mawasiliano wa Baraza la usalama wa taifa wa Marekani, John Kirby

Mratibu wa mawasiliano ya kimkakati wa Baraza la Kitaifa la Usalama nchini Marekani (NSC), John Kirby, Jumatatu alitetea uamuzi wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuvunja baraza la mawaziri la vita, na kusema kwamba hayo ni maamuzi ya ndani.

Netanyahu alivunja baraza hilo Jumatatu, uamuzi ambao ulitarajiwa baada ya Jenerali wa zamani Benny Gantz, mwanasiasa wa mrengo wa kati kuondoka katika baraza hilo wiki iliyopita.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari katika White House, Kirby alisema kwamba Netanyahu alikuwa na haki ya kuchukua hatua hiyo, na kusisitiza kuwa Rais Joe Biden ataendelea kufanya kazi pamoja na Netanyahu licha ya kutokubaliana kwao katika masuala fulani.

Gantz alijiunga na serikali ya umoja ya Netanyahu mwezi Oktoba wakati vita vilipoanza na aliomba liundwe baraza la vita. Netanyahu amelivunja baraza hilo bila Gantz kuwepo.

Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller aliwambia waandishi wa habari kwamba sio jukumu la Marekani kuamua nani anatakiwa kuwa katika serikali ya Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG