Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 02:15

Misri yalaumiwa kuwarejesha makwao wahamiji kutoka Sudan


Wasudani walaoishi Misri baada ya vita nchini mwao, wakisheherea tamasha la kiutamaduni huko Cairo Aprili 5, 2024. Picha na Ahmed HASAN / AFP
Wasudani walaoishi Misri baada ya vita nchini mwao, wakisheherea tamasha la kiutamaduni huko Cairo Aprili 5, 2024. Picha na Ahmed HASAN / AFP

Shirika la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limesema kuwa Misri imewakamata maelfu ya wahamiaji na kuwarejesha makwao, wengi wa wahamiaji hao wakiwa ni wale waliotoroka vita vya Sudan.

Shirika hilo limesema kuwa limeorodhesha visa 12 ambapo serikali ya Misri ilirejesha jumla ya raia 800 wa Sudan kati ya Januari na Machi mwaka huu, bila kuwapa nafasi ya kuomba hifadhi, au kujitetea dhidi ya kurejeshwa.

Ripoti zimeongeza kusema kuwa pia limeorodhesha kesi 27 za wakimbizi wa Sudan waliokamatwa kati ya Okotoba 2023 na Machi 2024, ishirini na sita wakiwa miongoni mwa wale waliofukuzwa nchini, baada ya kuzuiliwa kwenye mazingira magumu kabla ya kuondolewa nchini.

Idadi kamili ya watu waliokamatwa au kurejeshwa makwao haijulikani kwa kuwa hakuna takwimu zilizotolewa kwa umma, ingawa Human Rights Watch limesema kuwa maelfu walirejeshwa makwao mwishoni mwa mwaka jana, wengi wao wakiwa ni kutoka Sudan.

Wizara ya habari ya Misri bado haijatoa majibu kutokana na madai hayo. Kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, zaidi ya watu 500,000 ambao ni takriban asilimia 24 ya watu waliotoroka Sudan baada ya mapigano kuzuka, waliingia Misri.

Forum

XS
SM
MD
LG