Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 21:20

Jeshi la Sudan lauwa kamanda wa RSF, Darfur


Wanajeshi wa Sudan wakiwa kwenye uwanja wa vita kwenye jimbo la Northern State, karibu na mji wa Karima. Mei 19, 2024.
Wanajeshi wa Sudan wakiwa kwenye uwanja wa vita kwenye jimbo la Northern State, karibu na mji wa Karima. Mei 19, 2024.

Jeshi la Sudan limesema Ijumaa kwamba limemuua Ali Yagoub Gibril, kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la kijeshi la Rapid Support Forces, RSF, ambaye alikuwa amekewa vikwazo na Marekani, wakati wa mapigano kwenye mji uliozingirwa wa al-Fashir kaskazini mwa Darfur.

Gibril alikuwa kamanda mkuu wa RSF huko al Fashir, mji mkubwa wa mwisho katika mkoa wa Darfur nchini Sudan ambao haudhibitiwi na RSF. Jeshi la Sudan limesema katika taarifa kuwa Yacoub ameuliwa wakati shambulizi la RSF lilipozimwa mapema Ijumaa na wanajeshi wake na wale wa ushirika waliokuwa katika mapigano sambamba na wao kutoka makundi yaliyokuwa ya waasi yasio ya kiarabu kutoka Darfur.

RSF limekuwa likiuzingira al-Fashir, mji wenye wakazi milioni 1.8 kwa wiki kadhaa sasa, wakati maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wakionya kuwa ghasia hizo huenda zikapelekea kusambaa kwa ghasia za kijamii.

Forum

XS
SM
MD
LG