Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:55
VOA Direct Packages

Dharuba ya majira ya baridi Marekani yaua watu 34


Mkazi wa mkoa wa Buffalo huko Amherst, New York akiondoa theluji katika njia ya kuingiza gari nyumbani kwake, Desemba 25, 2022.
Mkazi wa mkoa wa Buffalo huko Amherst, New York akiondoa theluji katika njia ya kuingiza gari nyumbani kwake, Desemba 25, 2022.

Mamilioni ya watu walijifungia majumbani Jumapili ili kuepuka dhoruba ya majira ya baridi kali iliyouwa watu 34 kote nchini Marekani.

Dharuba hiyo inatarajiwa kusababisha vifo zaidi baada ya wakaazi wengi kukwama ndani ya nyumba zao kutokana na theluji.

Hali hiyo imesababisha umeme kukatika katika maelfu ya nyumba na biashara.

Dhoruba ambayo haikutarajiwa imekuwa kubwa kuanzia eneo la maziwa makuu karibu na Canada hadi Rio Grande kwenye mpaka na Mexico.

Karibu asilimia 60 ya watu nchini Marekani wamekabiliwa na fulani ya hali hiyo iliyosababisha maonyo ya hali ya hewa katika kipindi hichi cha baridi. Viwango vya hali ya hewa vimeshuka sana kuliko kawaida kutoka mashariki mwa milima ya Rocky hadi Appalachians, idara ya kitaifa ya hali ya hewa imesema.

Hali ya dharuba ya kipindi cha Baridi Marekani.
Hali ya dharuba ya kipindi cha Baridi Marekani.

Matatizo kwa wasafiri kutokana na hali ya hewa huenda yakaendelea , huku mamia ya safari za ndege zikifutwa na kunatarajiwa kutokea kimbunga kibaya sana - wakati kukiwa na shinikizo baya lakushuka kwa viwango vya hali ya hewa karibu na maziwa makuu, na kupelekea upepo mkali na theruji. Kulingana na tovuti inayofuatilia safari za ndege – Flightware. Baadhi ya safari za ndege takriban 1,707 za ndani na za kimataifa zilifutwa jumapili mchana.

Gavana wa New York Kathy Hochul amesema karibu kila gari la zimamoto kwenye mji humjini humo lilikwama Jumamosi , na aliwasihi watu kuheshimu marufuku iliyotolewa ya kutoendesha gari katika eneo hilo.

Gavana wa New York Kathy Hochul anaeleza:“ Bado tuko kwenye hali hii ya hatari sana na inayotishia maisha. Kwasababu tu watu wanaweza kuona mwanga kidogo leo, dhoruba hizo, upepo mkali , ukubwa wa hali hiyo, itarejea na itarejea usiku wa leo.kwa hiyo ujumbe wa kwanza nataka kusisitza kwa watu nilioko nao hapa leo, mnatakiwa kutokuwepo barabarani, tumekuwa tukiwaomba, tumekuwa tukiwaasa.”

Watabiri wa hali ya hewa wameonya kutakuwa na theruji nyingine itakayonyesha na ina uwezekano wa futi moja hadi mbili katika baadhi ya maeneo mapema jumatatu ikiambata na upepo wa kasi ya maili 40 kwa saa.

XS
SM
MD
LG