Tahadhari hizo zimeenea kutoka pwani hadi pwani na kufika kusini kabisa mwa mpaka wa Marekani na Mexico na Florida katika jimbo la Sunshine.
Viwanja vya ndege vikubwa vimefuta safari zake wakati dhoruba ikizidi kuwa mbaya.
Wakati dhoruba ikipiga eneo la maziwa makuu Alhamisi hali ya hewa ambayo inajulikana kama kimbunga bomu kilikuwa kinatarajiwa kushika kasi kwa katika shinikizo la chini linaloongezeka zaidi , huduma ya kitaifa ya hali ya hewa NWS imesema.
Kimbunga hicho kinaweza kusababisha kunyesha kwa theluji hadi nusu inchi kwa saa huku kukiwa na upepo unaovuma kutoka nyanda za juu za Magharibi Kati hadi eneo la Kaskaizini Mashariki na kusababisha upeo wa kuona ukawa karibu sifuri , idara ya hali ya hewa imesema.
Inawezekana umeme ukakatika kutokana na dhoruba yenye upepo mkali , theluji nyingi na barafu, ukichanganya na mahitaji makubwa ya nishati na dhoruba ilitarajiwa kusababisha baadhi ya nyakati usafiri kuwa wa shida.