Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 00:54

Jumla ya idadi ya watu Marekani yafika milioni 333.2, likiwa ongezeko la zaidi ya milioni moja kila mwaka.


Makazia ya watu kwenye mji wa Salt Lake City jimboni Utah
Makazia ya watu kwenye mji wa Salt Lake City jimboni Utah

Idara ya kitaifa ya hesabu ya watu hapa Marekani imesema Alhamisi kwamba idadi ya watu  nchini imeongezeka kwa kiwango cha watu milioni 1.2 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Hiyo ina maana kwamba sasa Marekani ina jumla ya watu milioni 333.2, ongezeko kubwa ikisemekana ni kutokana na wahamiaji. Tawkimu zinaonyesha kwamba watu wanaoingia Marekani kila mwaka imevuka ile ya wale wanaoondoka kwa milioni moja.

Takwimu pia zimeonyesha kwamba watoto takriban 245,000 zaidi wamezaliwa ikilinganishwa na idadi ya vifo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Baadhi ya majimbo kama vile California, New York, Oregon na Washington yanasemekana kupoteza wakazi waliohamia kwenye majimbo mengine.

Jimbo la Puerto Rico linaripotiwa kupoteza takriban wakazi 40,000 kutokana na uhamiaji au idadi ya vifo iliyopita ile ya uzazi.

XS
SM
MD
LG