Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:18

Chris Hani akumbukwa Afrika ya Kusini


Wanachama wa chama tawala cha African National Congress (ANC) na Chama cha South African Communist Party (SACP) wakipinga kuachiwa kwa Janusz Walus, aliyeshtakiwa kwa mauaji ya aliyekuwa katibu mkuu wa SACP Chris Hani, tarehe 10 Aprili 1993. Picha na Phill Magakoe / AFP.
Wanachama wa chama tawala cha African National Congress (ANC) na Chama cha South African Communist Party (SACP) wakipinga kuachiwa kwa Janusz Walus, aliyeshtakiwa kwa mauaji ya aliyekuwa katibu mkuu wa SACP Chris Hani, tarehe 10 Aprili 1993. Picha na Phill Magakoe / AFP.

Afrika Kusini siku ya Jumatatu iliadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya mwanaharakati aliyepinga ubaguzi wa rangi Chris Hani huku wito ukitolewa ukitaka uchunguzi mpya ufanyike kuhusu mauaji ambayo yalikaribia kuitumbukiza nchi vya rangi miaka 30 iliyopita.

Hani, ni mtu maarufu sana, alikuwa kiongozi wa chama cha Kikomunisti cha Afrika Kusini (SACP), aliuawa kwa kupigwa risasi na Janusz Walus, mbaguzi wa rangi, tarehe 10 Aprili, 1993.

Miongo mitatu baadaye, raia wengi wa Afrika Kusini wamekuwa na maswali kuhusu mauaji hayo, wakimshuku Walus na mshirika wake hawakufanya hivyo peke yao.

"Sina amani," mjane wa Hani, Limpho, aliwaambia watu waliohudhuria hafla hiyo ya kumbukumbu wakiwemo viongozi wa chama cha SACP na viongozi wa ngazi za juu kutoka nje siku ya Jumatatu.

"Ndio maana leo nimevaa nguo nyeusi. Naendelea kuomboleza mpaka wakati ambapo ukweli utakapodhihirika."

Wiki iliyopita, chama cha SACP kilitoa wito wa kufanyika uchunguzi mpya kuhusiana na mauaji hayo, na kutarajia kukusanya sahihi za watu 30,000.

"Kulikuwa na mambo mengi... ambayo hayakuchunguzwa ipasavyo," kiongozi wa SACP, Solly Mapaila aliliambia shirika la habari la AFP Jumatano. "Tunahitaji kuujua ukweli."

Akiwa na umri wa miaka 50, Hani aliuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake, mashariki mwa jiji la Johannesburg , mbelel ya binti yake aliyekuwa na umri wa miaka 15 wakati huo.

Tukio hilo lilisababisha maandamano na ghasia katika vitongoji vya watu weusi.

Hasira za watu weusi ambao ni idadi kubwa ya watu nchini Afrika Kusini ziliongezeka, Nelson Mandela alionekana kwenye televisheni ya taifa kuomba utulivu.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG