Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:39

Nyoka akutwa kwenye ndege Afrika ya Kusini


Watu wakimtafuta nyoka kwenye ndege huko Welkom, Afrika Kusini, tarehe 3 Aprili 2023. Picha na Brian Emmenis /AP.
Watu wakimtafuta nyoka kwenye ndege huko Welkom, Afrika Kusini, tarehe 3 Aprili 2023. Picha na Brian Emmenis /AP.

Rubani mmoja nchini Afrika Kusini Rudolf Erasmus ametua kwa dharura baada ya kugundua nyoka mwenye sumu kali aina ya kobra akiwa amejificha chini ya kiti chake.

Rubani Erasmus na abiria wanne kwenye ndege ndogo wakati akisafiri siku ya ya Jumatatu alihisi “kitu baridi” kikishuka kwenye sehemu ya chini ya mgongo wake. Alitazama chini kwa haraka na akaona kichwa kikubwa cha nyoka huyo aina ya Cape Cobra "kikirudi uvunguni mwa kiti," alisema.

"Ilikuwa kama vile ubongo wangu haukuwa ukitambua kilichokuwa kikiendelea," rubani huyo aliliambia shirika la habari la Associated Press.

Baada ya kufikiri kwa haraka, aliwajulisha abiria wake juu ya utelezi wa mzamiaji huyo.

"Kulikuwa na kimya cha kushangaza," alisema. Kila mmoja alitulia hususani rubani.

Erasmus alimpigia simu mdhibiti wa safari za anga ili kupata ruhusa ya kutua kwa dharura katika mji wa Welkom uliopo katikati ya nchi ya Afrika Kusini. Bado alilazimika kuendelea kuruka kwa dakika nyingine kati ya 10 hadi 15 na kutua akiwa na nyoka amejikunja miguuni mwake

“Niliendelea kumtazama kumuangalia yuko wapi. Alikuwa na furaha uvunguni mwa kiti," Erasmus alisema. "Huwa siogopi nyoka, lakini kwa kawaida siwakaribii."

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Associate Press

XS
SM
MD
LG