Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:54

Raia wa Afrika kusini aliyekutwa na mauaji baadae akatoroka amekamatwa Tanzania


Thabo Bester, raia wa Afrika kusini aliyekutwa na mauaji na baadae akatoroka nchini humo amekamatwa akiwa Tanzania
Thabo Bester, raia wa Afrika kusini aliyekutwa na mauaji na baadae akatoroka nchini humo amekamatwa akiwa Tanzania

Maafisa wa Afrika Kusini wanakwenda Tanzania kuanza mchakato wa kumrejesha Thabo Bester mwenye miaka 35 aliyejipa jina la "Mbakaji wa Facebook" wakati akitumia mtandao wa kijamii kuwarubuni wanawake angalau wawili ambao alipatikana nao na hatia ya kuwabaka

Raia wa Afrika Kusini aliyekutwa na hatia ya mauaji ambaye alidanganya kuhusu kifo chake ili atoroke gerezani amekamatwa nchini Tanzania kufuatia msako wa wiki mbili polisi wametangaza.

Maafisa wa Afrika Kusini wanakwenda Tanzania kuanza mchakato wa kumrejesha Thabo Bester mwenye miaka 35 aliyejipa jina la "Mbakaji wa Facebook" wakati akitumia mtandao wa kijamii kuwarubuni wanawake angalau wawili ambao alipatikana nao na hatia ya kuwabaka. Pia alipatikana na hatia ya kumuua mmoja. Bester alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2012 na iliripotiwa mwezi Mei mwaka jana kwamba alifariki kwa ajali ya moto iliyotokea katika gereza aliloshikiliwa.

Hata hivyo ripoti ziliibuka kuhusu yeye kuonekana mjini Johannesburg na uchunguzi ikiwemo sampuli za vinasaba (DNA) ulionyesha kuwa mwili uliopatikana umechomwa moto katika gereza hilo haukuwa wa Thabo Bester. Wiki mbili zilizopita polisi walisema walifuatilia mienendo ya Bester na wiki iliyopita walivamia nyumba ya kifahari ambayo inaaminika alipanga katika kitongoji cha watu matajiri huko Johannesburg.

Bester alikamatwa akiwa na mpenzi wake Nandipha Magudumana daktari maarufu anayehudumia watu mashuhuri na raia wa Msumbiji anayeaminika kuwasaidia kuvuka mpaka na kuwakimbia polisi maafisa walitangaza. Walipatikana na pasipoti kadhaa bandia ambazo hazikupigwa muhuri takriban kilomita 10 kutoka mpaka wa Kenya. Mamlaka hivi sasa zimeanza mchakato wa kuwarejesha watoro hao nchini Afrika Kusini mahala ambako wanatarajiwa kukabiliwa na mashtaka kadhaa.

Ujumbe rasmi kutoka Afrika Kusini unaojumuisha maafisa waandamizi kutoka polisi na idara ya sheria na huduma za urekebishaji unaelekea Tanzania Jumapili waziri wa Sheria Ronald Lamola alisema Jumamosi wakati akitangaza kukamatwa kwa Bester.

XS
SM
MD
LG