Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:31

Rubani Afrika ya Kusini apongezwa kwa ujasili wake


Afisa wa zimamoto akimsaka nyoka mwenye sumu kali ndani ya ndege, huko Welkom, Afrika Kusini, tarehe 3 Aprili, 2023. Picha na Brian Emmenis /AP.
Afisa wa zimamoto akimsaka nyoka mwenye sumu kali ndani ya ndege, huko Welkom, Afrika Kusini, tarehe 3 Aprili, 2023. Picha na Brian Emmenis /AP.

Rubani wa Afrika Kusini ambaye alitua kwa dharura baada ya nyoka mwenye sumu kutambaa na kuingia kwenye kiti chake amesifiwa na mamlaka siku ya Ijumaa kwa "kuonyesha ushujaa usio na kifani".

Rudolf Erasmus alikuwa akiendesha ndege ndogo binafsi mapema wiki hii akiwa na abiria wanne kutoka jiji la Bloemfontein kwenda Pretoria, wakati alipohisi nyoka mkubwa aina ya Cape Cobra akitembea mgongoni mwake.

Licha ya shinikizo kubwa, alitua bila tatizo huko Welkommji ulioko jirani na njiani kati ya miji hiyo miwili.

"Napenda kumpongeza Rudolf kwa hatua za kijasiri alizochukua na kwa jinsi alivyoshughulikia tukio hili ambalo lingeweza kuwa tukio baya la safari za anga," alisema mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Afrika Kusini (SACAA) Poppy Khoza.

“Alibaki kuwa mtulivu katika hali hiyo ya hatari na kuweza kutua salama bila kusababisha madhara yoyote kwake na abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo, na akiionyesha dunia kuwa yeye ni balozi wa usalama wa anga wa ngazi ya juu.”

Erasmus aliviambia vyombo vya habari kuwa alimgudua nyoka huyo akiwa katikati ya safari, baada ya kuhisi kitu cha baridi kikimkandamiza mgongoni.

"Kwanza nilifikiri ilikuwa chupa yangu ya maji... lakini baadaye nikagundua kuwa ni kitu kingine na (hivyo mimi) sikusogea," alikiambia kituo cha habari cha News24. Tukio hilo lilitokea Jumatatu.

Cape Cobra ni aina ya nyoka wenye wana sumu ya hatari ya neurotoxic ambayo inahitaji matibabu ya haraka ya dawa ya kuzuia sumu, nyoka hawa hupatikana sana maeneo ya kusini-magharibi mwa Afrika Kusini.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG