Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:24

Burundi yawaamuru maafisa wa WHO kuondoka nchini


Rais Pierre Nkurunziza, katikati, akiwasili katika mkutano mkuu wa chama tawala cha CNDD-FDD katika kijiji cha Gitega, Burundi, Jumapili, Jan. 26, 2020.
Rais Pierre Nkurunziza, katikati, akiwasili katika mkutano mkuu wa chama tawala cha CNDD-FDD katika kijiji cha Gitega, Burundi, Jumapili, Jan. 26, 2020.

Serikali ya Burundi imewaamrisha wawakilishi wa Shirika la Afya Duniani, WHO, na wataalam wengine wa afya, kuondoka nchini.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati wanasiasa nchini Burundi wanaendela na mikutano mikubwa ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu, licha ya onyo la wataalam wa afya likiwataka watu kutokaribiana katika juhudi za kudhibithi maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkuu wa ofisi ya WHO nchini Burundi Walter Kazadi Mulombo, pamoja na wataalam wengine watatu wa afya, wameandikiwa barua na serikali, wakitakiwa kuondoka nchini.

Afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Burundi, bila kutoa maelezo zaidi, amesema kwamba maafisa hao wa WHO, ni watu wasiotakiwa kuweto nchini humo.

Burundi inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu, Mei 20, kumchagua rais mpya atakayechukua nafasi ya Pierre Nkurunziza, mwenye historia ya kuwafukuza wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.

Mnamo mwaka 2018, wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, waliokuwa wakichunguza madai ya ukandamizaji wa haki za binadamu, walifukuzwa nchini humo.

Ripoti ya UN imevishutumu vyombo vya usalama na makundi ya wapiganaji ya chama kinachotawala Burundi, kwa kutekeleza vitendo vya kunajisi, mateso na mauaji.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG