Bunge la Msumbiji limeidhinisha mswaada wa sheria inayohalalisha kujihusisha kwa wanamgambo katika vita dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado.
Wanamgambo wa jimbo hilo wamekuwa wakisaidia jeshi na washirika wao kutoka Rwanda na Jumuia ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika katika vita dhidi ya wapiganaji wa kislamu katika jimbo hilo.
Waziri wa ulinzi Cristovao Chume aliyewasilisha mswaada huo bungeni amekiri kwamba jeshi la msumbiji halina uwezo wakutosha kupambana pekee yao na harakati za wapiganaji wa Kiislamu.
Anasema kuna haja ya dharura kubuni kikosi cha jimbo ili kuimarisha jeshi kuweza kupambana na kudhibiti kuenea kwa mashambulizi ya wapiganaji.