Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:52

Blinken asema Israeli Kamwe haitajitetea peke yake 'hasa kwa vile Marekani iko'


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiongea na wananchi alipotembelea kituo cha misaada kwa waathirika wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Hamas, Alhamisi Oct. 12, 2023, Tel Aviv. (AP Photo/Jacquelyn Martin, pool)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akiongea na wananchi alipotembelea kituo cha misaada kwa waathirika wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Hamas, Alhamisi Oct. 12, 2023, Tel Aviv. (AP Photo/Jacquelyn Martin, pool)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alisema leo Alhamisi Israel kamwe haitajitetea peke yake “hasa kwa vile Marekani iko.”

Alikuwa akiongea pembeni ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu katika mkutano wa wanahabari mjini Tel Aviv.

Blinken alisema Marekani itawapatia silaha za kuzuia silaha nyingine pamoja na kuisaidia kuboresha mfumo wake wa Israel wa iron Dome pamoja na vifaa vingine vya ulinzi.

Waziri wa Mambo ya Nje amesema:“Shehena nne za misaada ya kijeshi kutoka Marekani tayari zimewasili nchini Israel, na ziko njiani. Wakati mahitaji ya ulinzi ya Israel yanabadilika, tutafanya kazi na Bunge kuhakikisha kwamba yanatekelezwa. Naweza kukueleza, kuna idadi kubwa sana kubwa sana ya uungaji wa wote katika bunge letu kwa usalama wa Israel.”

Mwanzoni mwa mkutano huo wa waandishi wa habari, Blinken alisema kwamba amefika mbele ya wana habari “siyo tu kama waziri wa mambo ya nje, lakini pia kama myahudi wakati nikikumbuka historia ya familia yangu iliyonusurika na Holocaust.”

(FILES)Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken
(FILES)Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken

Blinken aliongeza kuwa:“Nimefika mbele yenu siyo tu kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, lakini pia kama myahudi. Babu yangu, Maurice Blinkeng, alikimbia vurugu zilizokuwepo Russia. Baba yangu wa kambo, Samuel Pisar alinusurika katika kambi aliyowekwa: Auschwitz, Dachau. Madjanek. Kwahiyo, waziri mkuu, naelewa binafsi kiwango cha vitisho vilivyofanywa na Hamas kuua Wayahudi wengi wa Israel, kwa kweli kwa Wayahudi kote kwingineko.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema kwamba “majeshi ya ustaarabu yatashinda,” huku kukiwa na mapigano na kulipiza kisasi kwa shambulizi baya sana la mwishoni mwa wiki lililofanywa na wanamgambo wa Hamas.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Netanyahu aliongeza kusema:“Kutakuwa na siku nyingi ngumu mbele yetu. Lakini sina shaka kwamba majeshi yetu ya kistraarabu yatashinda. Na kwa sababu hiyo ni kweli kwa vile tunaelewa nini hasa ni kipaumbele chetu cha kwanza katika ushindi, ni kama vile ulivyosema muda mfupi uliopita katika mkutano wetu, maadili ya uwazi. Huu ni wakati. Wakati mahsusi, wakati maalum ambao lazima tusimame kidete, tukijivuna na kuungana dhidi ya adui.”

Blinken pia atajaribu kusaidia kufikia muafaka wa kuachiliwa kwa watu waliotekwa na Hamas – baadhi yao ni Wamarekani – na kuendeleza mazungumzo kati ya Waisrael na Wamisri katika kutoa njia salama ya kupita kwa raia wa Gaza kutoka nje ya eneo hilo kabla ya uwezekano wa uvamizi wa ardhi wa Israel.

Baada ya Israel, Blinken ataelekea Jordan, ambako atakutana na Mfalme Abdulla na Rais wa Mamlaka ya Wapalestina, Mahmoud Abbas.

Ziara ya Blinken wakati Israel inafanya mashambulizi mazito sana ya mabomu katika historia ya miaka yake 75 ya mzozo na Wapalestina, ikiapa kuangamiza harakati za Hamas ambayo inatawala Ukanda wa Gaza ikiwa ni majibu kwa mashambulizi.

Israel imeiweka Gaza katika hali ya kuizingira na kuzuia upelekaji chakula na mafuta katika eneo hilo lenye watu takriban milioni 2.3.

Afisa mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje, akiongea na wana habari katika misingi ya kutotajwa jina, alisema Washington inafanya kazi ya kusukuma mbele mazungumzo kwa ajili njia ya salama ya kupita kwa raia, wakiwemo wamaekani ambao wako Gaza.

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Rais wa Marekani, Joe Biden akiongea na viongozi wa jamii ya Kiyahudi hapa Washington, Jumatano, alisema upelekaji wa manowari za kivita na ndege karibu na Israel kuonekane kuwa ni ishara kwa Iran, ambayo inaiunga mkono Hamas na harakati za Hezbollah nchini Lebanon.

“Tumeweka bayana kwa Wairan: muwe makini.” Alisema Biden.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG