Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:39

Israel yazidi kujiimarisha kupambana na Hamas


Israel, Jumatano imesema imeunda serikali ya dharura ya muungano ya wakati wa vita ili kupambana na wanamgambo wa Hamas, wakati huo huo ikikusanya wanajeshi 300,000 karibu na Gaza kwa kile kinachoweza kuwa uvamizi wa ardhini katika kanda hiyo ya Wapalestina.

Kwa upande wa ikulu ya Marekani, Rais Joe Biden alithibitisha uungaji mkono wa Washington kwa Israeli na kuwahakikishia kundi la viongozi wa Kiyahudi kwamba utawala wake unashughulikia kila nyanja ya mzozo pamoja na mateka nchini Israeli.

Ripoti zinasema baadhi ya Wamarekani wanaweza kuwa miongoni mwao jambo ambalo linaiunganisha Washington kwa kiasi kikubwa na mzozo huo.

Rais Biden hakutaka kueleza kwa kina juhudi maalum za kuwaokoa mateka, akisema, “kama ataweka wazi basa atashindwa kuwarejesha nyumbani.”

Amesema Marekani inatuma risasi, mifumo ya udhibiti, na ndege za kivita katika eneo hilo, pamoja na rasilimali muhimu kwa jeshi la wanamaji.

Forum

XS
SM
MD
LG