Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:00

Banki ya Dunia kuipa Kenya dola bilioni 12


Rais wa Kenya William Ruto akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Nairobi, Terehe 2 Aprili 2023. Picha na Tony KARUMBA/AFP.
Rais wa Kenya William Ruto akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Nairobi, Terehe 2 Aprili 2023. Picha na Tony KARUMBA/AFP.

Benki ya Dunia ilisema Jumatatu inatazamia msaada wa dola bilioni 12 kwa Kenya katika kipindi cha mitatu ijayo, utaliboresha taifa hilo la Afrika Mshariki ambalo linakabiliwa na matatizo ya kifedha.

Benki hiyo ilisema katika taarifa kwamba jumla ya pesa hizo zitatokana na idhini ya wakurugenzi watendaji wa benki hiyo na vigezo vingine ambavyo vinaweza kushawishi uwezo wake wa kukopesha.

Fedha za umma nchini Kenya zimeingiliwa kati na hali ya janga la COVID-19 na mabadiliko ya hali ya hewa ya mara kwa mara ikiwemo ukame.

“Benki ya Dunia imejitolea kikamilifu kuiunga mkono Kenya katika utekelezaji wake katika safari yake ya kuwa yenye kipato cha kati ifikapo 2030," ilisema taarifa hiyo.

"Kwa kuzingatia idhini ya Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Dunia kwa operesheni mpya , na kwa vigezo ambavyo vinaweza kuathiri uwezo wa benki kukopesha, hii inamaanisha jumla ya msaada wa fedha wa dola bilioni 12 katika kipindi cha miaka mitatu."

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia wa nchini Keith Hansen alisema dola bilioni 12 zikijumuisha pesa ambazo Kenya inazo kwa sasa kutoka kwenye Jumuiya ya Kimataifa ya Maendeleo, Benki ya Kimataifa ya Ujenzi na Maendeleo, Shirika la Kimataifa la Fedha na Wakala wa Kimataifa wa Dhamana ya Uwekezaji," pamoja na kile tunachotarajia kukitoa katika miaka mitatu ijayo."

"Hii inaweza kujumuisha Uendeshaji wa Sera ya Maendeleo pamoja na uwekezaji mpya katika sekta mbalimbali kama vile nishati, afya, usafiri na maji," Hansen alisema.

Kenya imekabiliwa na changamoto kubwa za ukwasi zinazosababishwa na kutokuwa na uhakika juu ya uwezo wake wa kupata ufadhili kutoka katika masoko ya kifedha kabla ya kukomaa kwa Eurobond ya dola bilioni mwezi Juni mwakani.

Forum

XS
SM
MD
LG