Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 02:26

Tanzania yatakiwa kutumia vizuri fursa za wageni wa kimataifa


Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Nairobi Novemba 14, 2023. Picha na SIMON MAINA / AFP.
Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Nairobi Novemba 14, 2023. Picha na SIMON MAINA / AFP.

Wasomi nchini Tanzania wamewataka viongozi nchini humo kutumia fursa za ziara mbalimbali za viongozi wa kimataifa wanaokuja nchini kujenga mahusiano mazuri katika kuendeleza diplomasia na ushirikiano wa kimataifa ili taifa hilo liweze kunufaika na ziara hizo.

Baadhi ya wasomi nchini humo waliyasema hayo wakati taifa hilo la Afrika Mashariki likitembelewa na rais wa Jamhuri ya Romania, Klaus Lohannis, kwa ziara rasmi ya siku nne.

Ukiwa ni muendelezo wa viongozi kutoka mataifa mbalimbali kuitembelea Tanzania suala linalo thibitisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na mataifa ya kigeni.

Wasomi wameshauri ili kupatikana manufaa ya ujio wa rais wa Romania, viongozi wa serikali wanapaswa kujenga mahusiano mazuri.

Prof Omary Fack kutoka Zanzibar ameeleza “kuna haja kwa serikali na viongozi walio karibu na Rais kujenga mahusiano na wale viongozi waandamizi ambao mheshimiwa Rais atafuatana nao, tunaweza kufaidika kielimu na kiuchumi kwa wasaidizi wa mheshimiwa Rais na viongozi wengine kujenga mahusiano mazuri na wale viongozi watafuatana na mheshimiwa Rais atakapokuja nchini kwetu.”

Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis akikagua gwaride la heshima katika Ikulu ya Nairobi
Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis akikagua gwaride la heshima katika Ikulu ya Nairobi

Tanzania na Romania zimekuwa zikishirikiana kwenye masuala mbalimbali ikiwemo biashara ambapo mwaka 2021 Tanzania iliuza bidhaa zenye thamani ya dola za Marekani million 7.9 ikilinganishwa na mwaka 2022 ambapo iliuza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 4.06 pekee ikionyesha kushuka kwa ushirikiano wa kibiashara kwa kipindi cha hivi karibuni.

Suala ambalo Balozi Samweli Shelukindo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema ziara hiyo inatarajiwa kuongeza fursa za masoko na biashara baada ya mikataba mbalimbali kusainiwa.

“Tuna matumaini makubwa kwamba ziara hii itafungua fursa kubwa sana za masoko na tunategemea kwamba vilevile kutasainiwa mikataba michache ya kuanzia kwa ajili ya kukuza mahusiano katika sekta ambazo tunafikiria tunaweza kupata faida kubwa” alisema Shelukindo.

Rais wa Kenya William Ruto akipomkaribisha Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis ikulu
Rais wa Kenya William Ruto akipomkaribisha Rais wa Romania Klaus Werner Iohannis ikulu

Akizungumza na Sauti ya Amerika Justine Kajerero Mchambuzi wa mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) amesema endapo yale yatakayozungumzwa na Marais hao yatatekelezwa kutakuwa na ongezeko la mnyororo wa thamani wa bidhaa, biashara pamoja na kilimo.

“Ni wazi kwamba mnyororo wa thamani wa biashara utakwenda mpaka kwenye kilimo, kwahiyo kwa ushirikiano huu maeneo kama ya samaki hasa minofu ya sangara ni vitu ambavyo vitapata nafasi kubwa katika biashara kati ya Tanzania na Romania endapo utekelezaji wa makubaliano na yale yatakayozungumzwa kati ya Marais hawa wawili yatatekelezwa vizuri.” alisema Kajerero.

Baada ya Rais huyo kuwasili nchini Tanzania anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake siku ya Ijumaa, tarehe 17 Novemba na kisha kuzungumza na waandishi wa habari kuelezea masuala muhimu yaliyojiri katika mazungumzo yao, na baadae atakwenda kukutana na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi tarehe 18 Novemba na kisha atakwenda kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mji mkongwe wa Zanzibar.

Imetayarishwa na Amri Ramadhani Sauti ya Amerika Dar es Salaam

Forum

XS
SM
MD
LG