Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:00

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yasitisha huduma za  usafirishaji mizigo Mombasa

Watembea kwa miguu wakijaribu kupita barabara iliyofurika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika wilaya ya Kiembeni mjini Mombasa mnamo Novemba 17, 2023.
Watembea kwa miguu wakijaribu kupita barabara iliyofurika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika wilaya ya Kiembeni mjini Mombasa mnamo Novemba 17, 2023.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi katika eneo la pwani ya Kenya yamesitisha huduma za  usafirishaji mizigo kwa njia ya reli kwenda na kutoka katika mji wa bandari wa Mombasa, shirika la reli la serikali lilisema Jumamosi.

Mvua kubwa ya El Nino, ikifuatiwa na mafuriko makubwa, imefunika miji kote Afrika Mashariki, na kuwaacha maelfu ya watu bila makazi.

Nchini Kenya, idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko ni takriban 46, na inatarajiwa kuongezeka.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi kwenye njia ya reli kati ya mji mkuu Nairobi na Mombasa yamelilazimu shirika la reli la Kenya kufunga huduma zote za mizigo, ilisema katika taarifa yake.

Reli hiyo pia husafirisha mizigo katika mataifa mengine katika kanda hiyo, ikiwa ni pamoja na Rwanda, Uganda na Sudan Kusini.

Forum

XS
SM
MD
LG