Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 07:52

Afrika Kusini yapambana na ongezeko la ukosefu wa ajira unaokaribia asilimia 33


Maandamano ya kushinikiza serikali ya Afrika Kusini iwawezeshe wananchi kupata ajira.
Maandamano ya kushinikiza serikali ya Afrika Kusini iwawezeshe wananchi kupata ajira.

Afrika Kusini inapambana na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira cha karibu asilimia 33. Umoja wa Mataifa na watalaamu wengine wameonya kwamba hili ni “bomu linalosubiri kulipuka” na  linaweza kusababisha ukosefu wa uthabiti wa kisiasa.

Janga halikusababisha matatizo kwa Themba Khumalo. Alipoteza ajira yake kama fundi mashine mwaka 2017 na hivi sasa anajaribu kuwasaidia mke wake na watoto wake wawili kwa kukusanya mabati na vitu vya plastiki popote anapoweza kuvipata na kuviuza kwa jumla ili vichakatwe.

“Jinsi ninavyoiona Afrika Kusini inakokwenda ni katika mwelekeo wa kiuchumi wa Zimbabwe. Itatulazimu kukimbia na kwenda nchi nyingine tukiwa na sifa zetu, na ujuzi wowote tulionao kwasababu serikali yetu haiwangaalii wanafunzi wa chuo kikuu katika misingi ya mustakbali wao. Ndiyo maana wanaondoka nchini kwa vile wanataka kuwa madaktari, au wauguzi au chochote. Wahitimu wanarudi nyumbani na kukaa bila ya kazi. Nailaumu serikali,” anasema Khumalo

Ana masikitiko jinsi anavyopata dola 18 kwa mwezi kama mafao kwa wasio na ajira ambazo hazimtoshi.

Zaidi ya nusu ya vijana nchini humo hawana ajira ikiwa ni matokeao ya kupanda kwa viwango vya umaskini na ukosefu wa usawa na matatizo ya kijamii kama vile uhalifu na matumizi ya dawa miongoni mwa vijana katika nchi yenye uchumi mzuri barani Afrika chini ya jangwa la Sahara.

Nchi imeombwa kufanya uingiliaji kati wa haraka kugeuza uchumi wake ili kujiepusha na viwango vya ukosefu wa ajira ambavyo vitafikia karibu asilimia 40 ifikapo mwaka 2030.

Steven Lesoona na Thabang Pule, wakusanya takataka, wakivuta matoroli yaliyosheheni takataka zinazopelekwa kuchakatuliwa wakikabiliana na uhaba wa ajira huko Naturena, karibu na Johannesburg, Afrika Kusini, Julai 3, 2023.
Steven Lesoona na Thabang Pule, wakusanya takataka, wakivuta matoroli yaliyosheheni takataka zinazopelekwa kuchakatuliwa wakikabiliana na uhaba wa ajira huko Naturena, karibu na Johannesburg, Afrika Kusini, Julai 3, 2023.

Mjini Pretoria, Lebohang Mphuthi mwenye umri wa miaka 26 anafanya kazi kama mwanafunzi msaidizi katika shule ya umma, miaka minne baada ya kuhitimu na kupata shahada katika uchambuzi wa kemia.

Ni kazi pekee ambayo ameweza kuipata, na majukumu yake yanahusisha kuwaangalia watoto wakati wa chakula cha mchana na kuwasaidia waalimu wakati wa madarasa.

Mphuthi anaelezea zaidi “unafahamu zile email ambazo mara nyingi zinasema” “tunasikitika kukujulisha kwamba maombi yako hayafukanikiwa.” ‘unaribu kubadilisha CV yako, unatumia mitindo tofauti na mambo mengi kama hayo lakini hakuna mafanikio. Ndiyo, niliomba kazi nyingi. Halafu mwaka jana, hapo ndipo nilipoomba kuwa msaidizi wa mwalimu. Niliona tangazo kwenye mtandao wa youth.mobi na nikasema wacha nijaribu.”

Katika muktadha wa Afrika Kusini, Mputhi huenda akaonekana kuwa ni mwenye bahati kwani analipwa dola 265 kwa mwezi.

Afrika Kusini ina kiwango kikubwa sana cha ukosefu wa ajira duniani, kwa mujibu wa Benki ya Dunia, wakiipita Gaza na Ukingo wa Magharibi, Djibouti na Kosovo.

Wachambuzi wanasema idadi rasmi ya ukosefu wa ajira haihesabu wale ambao wameacha kutafuta kazi na kuondoka katika gridi na kwamba tathmini sahihi zaidi huenda ikawa karibu asilimia 42 ya idadi ya watu walio katika umri wa kufanya kazi nchini Afrika Kusini hawana ajira.

Inapokuja ukosefu wa ajira kwa vijana, kiwango ni asilimia 61 kati ya wale walio na umri wa miaka 15 mpaka 24, kwa mujibu wa takwimu rasmi, na kiwango cha juu ni asilimia 71 kama ukihesabu tena wale ambao hawajaribu tena kutafuta ajira.

Pearl Pillay wa Youth Lab shirika ambalo linalenga katika kuboresha fursa kwa vijana amesema biashara mpya hazidumu au hata hazianzi na hazifanyi kazi.

“Ni ujuzi ambao hauna uwiano ambapo idadi ya vijana wote wamefikia umri wa kufanya kazi kwa wakati mmoja. Una hili kundi la vijana wapya wanaoingia katika soko la ajira. Hivi sasa, bahati mbaya, kwasababu hatuna uchumi unaokua, hakuna njia ya kuwatumia vijana wote waliopo. Halafu tunasema sehemu ya suluhisho ni kuwa wajasiriamali. Lakini pia tunaishi ndani ya mazingira ya kiuchumi ambayo hayatoi msaada unaostahili kwa ujasiriamali. Afrika Kusini ni moja ya sehemu ngumu sana kufanya biashara,” anasema Pillay.

Kuna hali ya kukata tamaa kwa mfano kitovu cha uchumi cha jimbo la Gauteng kilipoweka nia ya dhati ya kuajiri vijana 6,000 wasiokuwa na ajira katika nafasi mpya za kazi.

Zaidi viajan 40,000 walisimama nje kwenye baridi kali sana kuomba kazi, zaidi ya 30,000 walikataliwa. “Kwahiyo, una vijana milioni kumi ambao wamekaa nyumbani hawana hata hamu ya kutafuta kazi, hawana fursa ya elimu sahihi au mafunzo. Hiyo ni idadi ambayo itaendelea kuongezeka. Kwahiyo kuna hali ya kukata tamaa ambayo iko kwa vijana wadogo katika kutafuta kazi. Hatimaye utakuwa na uchumi ambao nguvu kazi yako itakuwa imetawaliwa na wazee ambao hatimaye watastaafu na umri utawatoa kwenye mchakato.”

Ikionya kuhusu ‘bomu linalosubiri kulipuka” huko Afrika Kusini kuhusu ukosefu wa ajira, Umoja wa Mataifa umekumbusha kuhusu wiki moja mwaka 2021 wakati ghasia na wizi uliposababisha zaidi ya watu 350 kufariki katika ghasia mbaya sana kuwahi kutoka tangu siku za mwisho za enzi ya ubaguzi wa rangi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG