Ghasia zilipungua mjini Cape Town baada ya mgomo wa wiki moja wa mabasi madogo ambao ulidumaza jiji hilo na kusababisha watu watano kufariki dunia akiwemo mtalii wa Uingereza polisi walithibitisha Alhamisi.
Mgomo huo ambao ulikwamisha wasafiri katika mojawapo ya miji mikubwa huko Afrika Kusini ulisitishwa Alhamisi jioni baada ya mazungumzo marefu. Hakuna vurugu mpya iliyoripotiwa tangu Jumanne.
Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 40 alipigwa risasi na kuuwawa Agosti 3 baada ya kufungwa kwa barabara na waandamanaji kumlazimisha kuendesha gari lake katika eneo la kitongoji kilichoshiriki mgomo huo.
Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na raia huyo wa Uingereza lakini uchunguzi bado unaendelea afisa wa Polisi Joseph Swartbooi aliiambia AFP.
Mtu huyo aliyetambuliwa kama Kar Teoh aliripotiwa kuuwawa mbele ya mkewe na mtoto wake wa kiume wa miaka miwili.
Forum