Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 17:42

Rais wa zamani wa Afrika Kusini apewa msamaha, aepuka kurudi tena jela


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (Kulia) na Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma Feb, 2018.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (Kulia) na Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma Feb, 2018.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ambaye alikaa miezi miwili tu jela kwa kifungo cha miezi 15 mwaka 2021, amepewa msamaha ulioidhinishwa na Rais Cyril Ramaphosa Ijumaa, akiepuka uamuzi ambao ungemfanya arudi tena jela.

Zuma alifungwa jela mwezi Julai 2021 kwa kukaidi amri ya mahakama kufika mbele ya tume ya uchunguzi kuhusu rushwa.

Aliachiliwa kwa sababu za kiafya baada ya miezi miwili, lakini uamuzi wa mahakama uliofikiwa na mahakama ya kikatiba uligundua uamuzi huo kuwa kinyume cha sheria.

Mkuu wa huduma za magereza wa Afrika Kusini alitarajiwa wiki hii kutangaza iwapo Zuma atarudi jela. Msamaha uliotolewa Ijumaa unaelekea kubatilisha uamuzi huo wa kurudishwa jela.

Kufungwa kwa Zuma mwaka 2021 kuliibua maandamano yenye ghasia ambapo zaidi ya watu 300 waliuawa, na kulikuwa na hofu kuwa iwapo atarudishwa jela kungetokea ghasia zaidi.

Kamishna wa taifa wa huduma za magereza wa Afrika Kusini, Makgothi Samuel Thobakgale, aliwaambia waandishi kuwa Zuma alifika kenye gereza la Estcourt kwa kiasi cha saa moja Ijumaa asubuhi katika jimbo la KwaZulu-Natal (KZN) mji anakotokea ambako alikuwa amefungwa mwaka 2021.

Maafisa wa magereza wanaendelea kuwasiliana na Zuma, kama wanavyofanya kwa wahalifu wengine ambao wanapitia mchakato wa msamaha, Kamishna huyo aliongeza kusema.

Jacob Zuma akiwa mahakamani Januari 31, 2022.
Jacob Zuma akiwa mahakamani Januari 31, 2022.

Chama kikubwa cha upinzani, Democratic Alliance, kilisema katika taarifa yake kuwa kinapanga kuwasilisha changamoto ya kisheria dhidi ya uamuzi huo wa kumpa msamaha maalum Zuma.

Msemaji wa Taasisi ya Zuma alisema kuwa Zuma alikuwa nyumbani akishauriana na timu yake ya wanasheria na taarifa huneda ikatolewa baadae.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG