Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:57

Afrika Kusini yacharaza Italy kwenye kombe la Dunia la Wanawake-WWC


Picha ya baadhi ya wachezaji wa timu ya wanawake ya Afrika Kusini
Picha ya baadhi ya wachezaji wa timu ya wanawake ya Afrika Kusini

Thembi Kgatiana alifunga goli la mapema Jumatano na kuipa Afrika Kusini ushindi wa 3-2 dhidi Italy na  hivyo kufuzu kuingia kwenye duru ya mtoano kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia la wanawake.

Kwenye usiku uliojawa na mbwembwe pamoja na viwango vya chini vya joto, Hilda Magaia alifunga bao katika dakika ya 67 na kuiweka Afrika Kusini kuongoza 2-1 dhidi ya Italy, kabla ya Arianna Caruso kusawazisha na kuwa na sare ya mbili kwa mbili, na hivyo kwa muda kidogo na kuzima matumaini ya Afrika Kusini.

Iwapo mechi hiyo ingeishia kwa sare, basi Italy ambayo ipo kwenye nafasi ya 8, ingeingia kwenye raundi ya mtoano. Afrika Kusini sasa itacheza na Uholanzi kwenye raundi ya 16 bora Jumapili. Sweden ilimaliza ikiwa kwenye nafasi ya kwanza katika kundi G baada ya kuicharaza Argenitina 1-0 na sasa itakumbana na mabingwa watetezi Marekani kwenye mechi ijayo.

Forum

XS
SM
MD
LG