Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 21:10

Afrika Kusini kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Wanawake Jumatano


Wanawake wa Afrika Kusini wakivalia mavazi ya kitamaduni katika mji wa Nongoma, Aug. 20, 2022.
Wanawake wa Afrika Kusini wakivalia mavazi ya kitamaduni katika mji wa Nongoma, Aug. 20, 2022.

Wakati zaidi ya wanawake 10,000 wakibakwa katika miezi ya tatu ya kwanza ya mwaka huu pamoja na wengine 900 kuuawa nchini Afrika Kusini, wataalam wanasema kwamba hakuna kikubwa cha kusherehekea Jumatano wakati nchi hiyo inapoadhimisha Siku ya Kitaifa ya Wanawake.

Siku ya Wanawake inayoadhimishwa Agosti 9 kila mwaka Afrika Kusini, ni kumbukumbu ya kitaifa ya maandamano ya kihistoria kupinga sheria kandamizi za kibeberu dhidi ya wanawake.

Takwimu za polisi katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu zimeonyesha kwamba kulikuwa na visa 10,512 vya ubakaji na 969 vya mauaji. Rais wa Afrika Kusin Cyril Ramaphosa amesema kwamba ukatili wa kijinsia unaoshudiwa nchini mwake unaweza tu kulinganishwa na mataifa yaliopo vitani, akiliita janga la kitaifa.

Forum

XS
SM
MD
LG