Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 10:51

Jacob Zuma wa Afrika kusini ameachiliwa huru baada ya kujisalimisha gerezani


Rais wa zamani wa Afrika kusini, Jacob Zuma akiwa mjini Johannesburg. Oct. 22, 2022.
Rais wa zamani wa Afrika kusini, Jacob Zuma akiwa mjini Johannesburg. Oct. 22, 2022.

Aliachiliwa kwa sababu za kiafya. Kuonekana kwake Ijumaa kunaweza kumrudisha gerezani ili amalize kifungo chake lakini badala yake alipewa msamaha, ambao unampunguzia kumaliza kifungo chake kilichosalia

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameachiliwa huru Ijumaa baada ya kujisalimisha kwenye gereza moja katika jimbo lake la KwaZulu-Natal. Zuma alikuwa amehukumiwa kifungo cha miezi 15 jela mwaka 2021 kwa tuhuma za rushwa lakini alikaa gerezani kwa miezi miwili tu.

Aliachiliwa kwa sababu za kiafya. Kuonekana kwake Ijumaa kunaweza kumrudisha gerezani ili amalize kifungo chake lakini badala yake alipewa msamaha, ambao unampunguzia kumaliza kifungo chake kilichosalia. Mpango huo wa msamaha ulioidhinishwa na Rais wa sasa wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa umelenga kupunguza idadi ya wafungwa walio katika kiwango cha chini cha hatari huko Afrika Kusini.

Kufungwa kwa Zuma mwaka 2021 kulizusha maandamano ya wiki kadhaa ambapo watu 300 waliuawa. Mahakama ilieleza kuachiliwa kwake kutoka gerezani mwaka 2021 ni kinyume cha sheria. Hata hivyo, rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 81 aliachiliwa huru kutoka kizuizini siku ya Ijumaa baada ya takribani saa mbili.

Chama kikuu cha upinzani cha Democratic Alliance nchini Afrika Kusini, kimesema kitaweka changamoto juu ya kuachiliwa kwa rais huyo wa zamani.

Forum

XS
SM
MD
LG