Hayo yalifuatia maandamano kama hayo, yaliyofanyika Jumatano mjini Nairobi, ambayo kwa kiasi kikubwa yaliwajumuisha vijana.
Serikali ya Rais William Ruto inayokabiliwa na uhaba wa fedha, ilikubali kubadilisha baadhi ya mapendekezo kwenye rasimu ya mswada huo, baada ya shinikizo kutoka kwa Wakenya.
Hata hivyo, walioingia mitaani hii leo, wanasema mabadiliko hayo hayatoshi. Maandamano hayo yalifanyika katika miji kama Nairobi, Mombasa, Eldoret na Kisumu, baadhi zikiwa ni ngome za upinzani, wakiwataka wabunge kuukataa mswada huo.
"Wanahitajika kukataa mswada huo, siyo kuuhariri," Sarah Njoroge, 21, aliliambia shirika la habari la AFP.
"Inaonekana wanafikiri tunazungumza tu kwenye mitandao ya kijamii na kwamba tutachoka," aliongeza.
"Jumatano, serikali ilifunga barabara kadhaa karibu na bunge jijini Nairobi na kusambaza polisi wengi, huku wabunge wakiendelea na mjadala kuhusu mswada huo.
Kodi hizo zilitarajiwa kuongeza dola bilioni 2.7, sawa na asilimia 1.9 ya Pato la Taifa, na kupunguza nakisi ya bajeti kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 3.3 ya Pato la Taifa.
Forum