Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:09

Rwanda yaituhumu DRC imekodi mamluki


Rais wa DRC Felix Tshisekedi, kushoto, na Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa DRC Felix Tshisekedi, kushoto, na Rais wa Rwanda Paul Kagame

Mzozo unaofukuta Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, umeikumba Russia na nchi nyingine za Ulaya Mashariki ambazo zinatuhumiwa kuisaidia Kinshasa kwa kuwapatia mamluki.

Rwanda, jirani wa Kinshasa anayeonekana kuwa ni mchokozi na kushutumiwa vikali kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 katika mapigano yao dhidi ya serikali ya Felix Tshisekedi, imeishutumu serikali ya Kongo kwa kujiandaa kwa vita badala ya kupunguza mivutano sambamba na juhudi mbalimbali za kuleta amani zinazoendelea.

Kigali siku zote imekuwa ikikana kujihusisha na waasi.

Alhamisi, utawala wa Paul Kagame ulitoa taarifa fupi ambayo haikufurahisha ikidai kuwa Kinshasa imeagiza mamluki kutoka nje kuwasaidia vita vyake dhidi ya M23.

M23, katika taarifa tofauti iliyotolewa siku hiyo hiyo ilirejea kusema wapo mamluki kwa hisani ya serikali hiyo.

Mpaka wakati habari hii inakwenda kuchapishwa, Kinshasa haijajibu madai haya. Mivutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imepamba moto na mahusiano yamepungua kwa kiasi kikubwa, huku Kigali ikimtuhumu jirani yake kwa kuhujumu juhudi zinazoendelea za kikanda za kuleta utulivu katika eneo la mashariki mwa nchi.

Endapo itajulikana kama kampuni ya mamluki ya Russia, Wagner Group imeweka kambi DRC , hii inaweza kuleta mkanganyiko katika mzozo, ambapo taasisi za kikanda — EAC na Mkutano wa Kimataifa wa Kanda ya Maziwa Makuu (ICGLR) — ambao wanajaribu kuutatua mgogoro huu.

Taarifa kuhusiana kuwepo kwa mamluki pia zimeelezwa kwa kina katika ripoti ya Umoja wa Mataifa, ambayo iliwataja Waromania, Wabulgaria, Wageorgia na Wabelarusi - wa Ulaya ambao kiasili wana uhusiano wa karibu na Russia – ni miongoni mwa wale walioonekana huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Kundi la Wagner, kampuni ya binafsi ya kijeshi iliyoanzishwa na Yevgeny Prigozhin, aliyekuwa msaidizi wa rais wa Russia Vladimir Putin ambaye pia anajulikana kwa jina la “Putin’s Chef,” ametajwa sehemu mbalimbali barani Afrika akiendesha shughuli zake katika maeneo yenye mizozo ikiwemo Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan na kwa muda mfupi nchini Msumbiji.

XS
SM
MD
LG