White House yajizuia kujadili kesi ya Trump

Rais wa Marekani Joe Biden

Wakati mtangulizi wake akiwa anaieleza mahakama kuwa hana makosa kwa madai ya uhalifu wa juu mahakamani, Rais wa Marekani Joe Biden alikutana na washauri wake wa sayansi na teknolojia.

Rais Biden ameeleza hatari na faida za programu ya teknolojia maarufu kama Artificial Intelligence. Hata hivyo alipuuza maswali ya waandishi kuhusu Trump kufunguliwa mashtaka.

Rais wa zamani Donald Trump akiwa mahakamani New York.

Rais Jumanne hakuwa anafuatilia shughuli zilizokuwa zinaendelea New York, kulingana na msemaji wa White House Karine Jean-Pierre.

“Ni kesi inayoendelea, na hivyo hatutaingia kutoa maoni kuhusu kesi hiyo,” alisema Jean-Pierre. “Angalia, rais atalenga tu mambo ya watu wa Marekani kama anavyofanya kila siku.”

Kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer alitoa taarifa akisema anaamini kuwa Trump atapata kesi ya haki kuhusiana na makossa 34 ya uhalifu kwa kughushi nyaraka za biashara zinazohusishwa na malipo ya fedha za kumnyamazisha mwanamke.

Chuck Schumer

Wabunge kadhaa wa Republikan wanaliangalia hilo kwa njia tofauti. Wanaiita kesi hiyo dhidi ya rais wa zamani ni kesi yenye ushawishi wa kisiasa.

Imetayarishwa na mwandishi wa VOA Steve Herman, Washington DC.