Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan akamatwa

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan

Fawad Chaudhry, afisa mwandamizi wa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf alisema Khan, mwenye umri wa miaka 72, alikamatwa Jumanne kwenye majengo ya mahakama na maafisa kutoka taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo.

Khan aling’olewa mamlakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye, mwezi Aprili mwaka jana.

Amedai kufukuzwa kwake kulikuwa kinyume cha sheria na njama za mataifa ya Magharibi, na amefanya kampeni dhidi ya serikali ya mrithi wake, Waziri Mkuu Shahbaz Sharif, akitaka uchaguzi wa mapema.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 alikamatwa wakati akielekea katika chumba cha mahakama kuu ambako dazeni za kesi zinazomkabili kuanzia madai ya ugaidi, ufisadi, uhaini na makosa mengine ya jinai, zilikuwa zianze kusikilizwa.

Mawakili wa Khan walidai kuwa vikosi vya wanamgambo vilimshambulia kabla ya kumweka chini ya ulinzi na kumkabidhi kwa maafisa wa kupambana na ufisadi walioambatana nao.