Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:00
VOA Direct Packages

Wahamiaji 55 waripotiwa kufa kwenye bahari ya Mediterranean, baada ya boti yao kupinduka karibu na Libya


Wahamiaji kutoka mataifa tofauti wakiwa kwenye boti katika bahari ya Mediterranean. picha ya maktaba.
Wahamiaji kutoka mataifa tofauti wakiwa kwenye boti katika bahari ya Mediterranean. picha ya maktaba.

Shirika la Uhamiaji  la Umoja wa Mataifa,IOM, limesema Jumatano kwamba boti iliyotengenezwa kwa mpira, iliyokuwa imebeba darzeni ya watu waliokuwa  wakielekea Ulaya ilizama karibu na ufukwe wa Libya na kuuwa takriban watu 55.

Miongoni mwa waliokufa ni wanawake na watoto, ikiwa ajali ya karibuni zaidi kwenye bahari ya Mediterranean, ambayo hutumika kama njia ya wahamiaji wanaotaka kuingia Ulaya wakitokea Afrika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, shirika la UN la Uhamiaji , IOM, limesema kwamba ajali hiyo ilitokea Jumanne, wakati boti hiyo ikiwa imebeba wahamiaji 60 , ikitokea mwenye mji wa bandari wa Garabouli, mashariki mwa mji mkuu wa Libya wa Tripoli.

IOM limesema kwamba wahamiaji 5 waliokolewa kutoka kwenye boti hiyo na kupelekwa kwenye ufukwe na walinzi wa pwani wa Libya. Haijabainika hasa kilichosababisha ajali hiyo.

Msemaji wa IOM, Safa Msehli amesema kwamba boti hiyo ilipinduka muda mfupi baada ya kuondoka Garabouli, akiongeza kwamba kufikia Jumatano, miili 9 ya wanaume ilikuwa imepatikana, pamoja na mtoto mmoja.

Waliyookolewa ni wanaume 4, watatu wakiwa raia wa Pakistan na mmoja kutoka Misri, pamoja na mtoto mmoja kutoka Syria. IOM limesema kwamba takriban watu 537 wamekufa maji au kutoweka katika ajali zinazohusishwa boti za wahamiaji, kwenye bahari ya Mediterranean, karibu na ufukwe wa Libya mwaka huu, huku wengine zaidi ya 4,300 wakikamatwa na kurejeshwa kwenye ufukwe.

Mapema mwezi huu, mradi wa wahamiaji waliopotea wa IOM, ulisema kwamba katika robo ya kwanza ya mwaka huu, kulikiwa na takriban vifo 441 vya wahamiaji kwenye bahari ya Maditerranean, kikiwa kiwango kikubwa zaidi tangu 2017.

XS
SM
MD
LG