Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:05

Pakistan imeamua kumrejesha balozi wake nchini Afghanistan


Waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Bilawal Bhutto Zardari (L) na Waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan, Amir Khan Muttaqi. Apr. 16, 2023.
Waziri wa mambo ya nje wa Pakistan Bilawal Bhutto Zardari (L) na Waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan, Amir Khan Muttaqi. Apr. 16, 2023.

Uamuzi huo ulitokana na mazungumzo ya simu ya usiku kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Bilawal Bhutto Zardari na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi. Balozi anatarajiwa kuwasili Kabul kabla ya sikukuu za Eid-ul-Fitr

Pakistan imeamua kumrejesha balozi wake nchini Afghanistan wiki hii zaidi ya miezi minne baada ya kuondolewa kwa sababu ya jaribio lililofeli kutaka kumuua mjini Kabul lililofanywa na kundi la Islamic State vyanzo kadhaa rasmi vimeiambia VOA Jumapili.

Uamuzi huo ulitokana na mazungumzo ya simu ya usiku kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Bilawal Bhutto Zardari na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi. Balozi anatarajiwa kuwasili Kabul kabla ya sikukuu za Eid-ul-Fitr afisa wa serikali ya Pakistan alisema akiomba jina lake lisitajwe kwa sababu hana mamlaka ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Afisa huyo alikataa kutoa maelezo zaidi akisema harakati za kidiplomasia zinahitaji usiri kwa sababu za kiusalama. Sherehe za siku tatu za Eid za kuadhimisha kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan zinatarajiwa kuanza nchini Afghanistan wikiendi hii.

XS
SM
MD
LG