Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:00
VOA Direct Packages

Tetemeko la ardhi lazua hali ya taharuki Pakistan na Afghanistan. Mamia hospitalini kutokana na mshtuko


Picha ya maktaba ya tetemeko la ardhi la Pakistan
Picha ya maktaba ya tetemeko la ardhi la Pakistan

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.5 kwenye vipimo vya rikta limetikisa sehemu kubwa ya Pakistan na Afghanistan Jumanne na kupelekea wakazi waliokumbwa na wasiwasi kuondoka kwenye nyumba zao pamoja na ofisi.

Hofu pia ilitanda kwenye maeneo ya vijiji, wakati watu wawili wakisemekana kufa kutokana na tukio hilo. Zaidi ya watu 100 walipelekwa hospitalini kutokana mshtuko kwenye bonde la Swat, lililopo kwenye jimbo la kaskazini magharibi mwa Pakistan la Khyber, kulingana na Bilal Faizi ambaye ni msemaji wa huduma za dharura za taifa hilo, akizungumza na shirika la habari la AP.

Taimoor Khan ambaye ni msemaji wa timu ya dharura ya jimbo hilo amesema kwamba nyumba kadhaa zilizotengenezwa kwa matofari ya udongo ziliporomoka kweye maeneo ya vijijini. Tetemeko hilo pia linasemekana kusababisha watu wengi kuondoka nyumba zao pamoja na ofisi kwenye mji mkuu wa Pakistan wa Islamabad. Ripoti kutoka kwa vyombo vya habari zinasema kwamba baadhi ya nyumba za makazi mjini humo zilipata nyufa.

XS
SM
MD
LG