Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Kenya Monica Juma alisema kikosi hicho kitaweka kipaumbele katika kuwalinda raia, kuruhusu watu kutembea, na kuwepo njia za usafiri wa bidhaa na misaada ya kibinadamu, na kulinda taasisi za serikali.
Kikosi hiki cha kulinda amani kilichokuwa kikisubiriwa kwa muda mrefu, kinachoongozwa na Kenya kiliwasili katika nchi ya Caribbean mnamo Jumanne (Juni 25).
Vita vya magenge nchini Haiti sasa vimewakosesha makazi watu nusu milioni.
Takriban watu milioni tano wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Makundi yenye silaha, ambayo sasa yanadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu, yameunda muungano mpana huku yakitekeleza mauaji yaliyoenea, utekaji nyara na unyanyasaji wa kingono.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari