Lieberman ni kati ya wale walioko katika serikali ya Israeli na sehemu nyingine ambao walikosoa suluhishi lililosimamiwa na Misri, wakipendelea badala yake majeshi ya Israeli kutumia mabavu zaidi kukabiliana na wapiganaji hao katika Ukanda wa Gaza.
Amesema Jumatano kuwa makubaliano hayo ni “kujisalimisha kwa ugaidi.”
Muda mchache hapo awali, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alitetea uamuzi wa kusitisha mapigano katika Gaza na kumaliza siku kadhaa za mapigano hatarishi kati ya pande hizo mbili.
“Maadui zetu wameomba tufikie suluhu ya kusitisha mapigano na wanajua kwani nini,” amesema Netanyahu.
Wapiganaji huko Gaza walipiga makombora na mabomu nchini Israeli, lililosababisha Israeli kufanya mashambulizi ya anga na kulenga maeneo 160 huko Gaza.
Haya ni mapigano makali ambayo hajawahi kutokea katika kipindi cha muda wa miaka minne.