Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 08:48

Polisi wapendekeza Netanyahu kufunguliwa mashtaka


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akitoa hotuba huko Jerusalem. Feb. 13, 2018.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akitoa hotuba huko Jerusalem. Feb. 13, 2018.

Polisi wa Israel walipendekeza Jumanne kwamba Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu afunguliwe mashtaka kwa shutuma za rushwa.

Kashfa hiyo imesababisha msukosuko wa kisiasa kwenye taifa hilo na kupelekea kuibuka maswali juu ya iwapo muda wake mrefu wa kuwepo madarakani unakaribia kikomo.

Netanyahu ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa taifa la Israel kwa takribani miaka 12 alilihutubia taifa wakati habari za mapendekezo hayo zinatolewa na hivyo kuweza kutangaza rasmi hadharani na kuweka bayana kwamba hana nia ya kujiuzulu.

Alisema katika hotuba yake kupitia televisheni akiwa amesimama mbele ya bendera nne za Israel huku akionekana hana furaha.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu

“Katika kipindi cha miaka kadhaa sasa, nimekuwa nikikabiliwa na angalau uchunguzi wa shutuma 15 kwa lengo la kuniondoa madarakani. Baadhi yamekua ni mapendekezo mabaya ya ajabu kama yanayoelezwa usiku huu na polisi. Majaribio yote hayo hayakuzaa matunda na kwa mara nyingine tena watakosa kile wanachokitaka”.

Uamuzi wa iwapo anafunguliwa mashtaka hivi sasa upo mikononi mwa ofisi ya mwanasheria mkuu, uamuzi ambao unatarajiwa kuchukuliwa katika muda wa wiki au miezi kadhaa juu ya namna ya kusonga mbele na suala hilo.

Waziri mkuu anayekabiliwa na mapendekezo ya aina hiyo kutoka polisi au ambaye amefunguliwa mashtaka rasmi hatakiwi kujiuzulu. Polisi walisema katika taarifa kwamba walikuwa wakipendekeza mashtaka rasmi juu ya hongo, wizi na kupoteza imani ya umma.

Polisi wamekuwa wakimchunguza Netanyahu kutokana na wasiwasi ambapo yeye na familia yake walipokea zawadi za gharama kutoka kwa mzalishaji wa Hollywood, Arnon Milchan pamoja na bilionea mmoja wa Australia, James Packer. Zawadi hizo zinashutumiwa kuhusisha SIGA, dhahabu na shampeni zenye thamani. Kulingana na taarifa ya polisi inakadiriwa kwamba jumla ya gharama ya zawadi zilizopokelewa kati ya mwaka 2007 na 2017 ni kiasi cha dola 283,000

Pia wanachunguza shutuma kwamba Netanyahu aliomba mkataba wa siri wa kumtangaza mchapishaji anayefanya mauzo ya juu ya magazeti, Yediot Aharonot.

Polisi kwenye taarifa yao pia walipendekeza kumfungulia mashtaka ya hongo Michan na mchapishaji Arnon Moses.

Bwana Netanyahu alisema katika hotuba yake akielekeza kwenye kesi inayomuhusu mwenyewe. “Mapendekezo hayo hayana thamani yeyote ya sheria katika nchi yenye demokrasia, sisemi hivyo kwa kukejeli, ninasema hivyo ili kusisitiza sheria za msingi katika demokrasia yetu, Israel ni taifa la kidemokrasia, taifa linalofuata sheria na kulingana na sheria, sio polisi ambaye anaamua, ni jopo la sheria pekee ndio lenye mamlaka hayo. Serikali yetu itamaliza muhula wake na nina uhakika kwamba katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika 2019, kwa mara nyingine nitashinda tena bila wasi wasi”.

Avi Gabbay, kiongozi wa upinzani huko Israel
Avi Gabbay, kiongozi wa upinzani huko Israel

Wakati huo huo Avi Gabbay kiongozi wa upinzani wa chama cha Labour alisema kwamba enzi za Netanyahu zimekwisha.

“Ni jukumu la kila kiongozi mwenye heshima kwa umma kuboresha sera na sheria na pia kuchukua hatua kumaliza mtazamo wa serikali inayoongozwa na Netanyahu”, aliandika kwenye Twitter.

XS
SM
MD
LG