Watu tisa wauawa katika mzozo wa aridhi DRC

Mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

Watu tisa wamefariki dunia kutokana na shambulizi lililotokea jirani na Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako makabila mawili yamejikuta katika mzozo mkubwa wa ardhi, wanakijiji na afisa wa usalama alisema.

Shambulio hilo lilitokea siku ya Jumapili katika jimbo linalopakana na jimbo la Mai-Ndombe, ambapo kulingana na wa Shirika la Human Rights Watch (HRW) kuna watu takriban 300 wamekufa na zaidi ya 50,000 kuyakimbia makazi yao tangu Juni mwaka jana.

Mgogoro huo unaowapinga watu wa kabila la Teke, ambao wanajiona kihistoria kuwa ni wazawa wa eneo hilo la kilomita 200 lililoko kwenye ukingo wa mto Congo, wanasema kabila la Yaka ambao Teke wanasema waliwasili eneo hilo baada ya wao kuwasili.

Kundi lenye silaha lilifanya shambulizi hilo kabla ya alfajiri katika kijiji cha Yosso, ambapo "watu tisa waliuwawa, wakiwemo watoto wawili,"kulingana na Reagan Mangawana, ambaye anatoka kwenye kijijini hicho, na kusema alikwenda kijijini pale akitokea nyumbani kwake mjini Kinshasa siku ya Jumatatu.

Katika shambuliao hilo, watu watano walijeruhiwa vibaya na eneo la kusini mwa kijiji hicho iliteketezwa kwa moto, Mangawana, aliliambia shirika la habari la AFP Jumatatu jioni.

Afisa wa usalama alithibitisha idadi ya watu tisa waliofariki.

Miili sita ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Ndjili iliyoko mashariki mwa mji wa Kinshasa, lakini "mingine mitatu ilikuwa vipande vipande... na haikuweza kuungika," aliongeza Jean Bedel Mulele, chifu wa jadi wa kijiji jirani cha Kie.

Kwa kiasi kikubwa mzozo huo unaoendelea wa Mai-Ndombe umekuwa ukipuuzwa na nchi nyingine mbali na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati nchi za jirani zikizingatia matatizo ya miongo kadhaa yaliyoko mashariki mwa nchi hiyo.

Mzozo mwingine wa ardhi, unaopinga makundi ya Mbole na Lengola ulitokea Kisangani katikati-mashariki mwa nchi hiyo, ambapo watu takriban wanne waliuawa katika mapigano hayo yaliyotokea wiki iliyopita.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP .