Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:57

Vifo kutokana na mafuriko DRC vimeongezeka na kufikia zaidi ya 400


Wakaazi huko DRC wakiomboleza vifo kutokana na mafuriko ya wiki iliyopita
Wakaazi huko DRC wakiomboleza vifo kutokana na mafuriko ya wiki iliyopita

Serikali ya Congo imetangaza leo jumatatu siku ya kitaifa ya maombolezo. Maafisa nchini DRC wanasema watu wengi bado hawajulikani walipo. Mvua kubwaz ilinyesha hasa kwenye vijiji vya Bushushu na Nyamukubi.

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko ya wiki iliyopita huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeongezeka na inaelezewa ni zaidi ya 400. Maafisa wanasema watu wengi bado hawajulikani walipo.

Mvua kubwa ilinyesha hasa kwenye vijiji vya Bushushu na Nyamukubi. Idadi ya watu waliokufa inawalazimisha wanavijiji kuwazika walifoariki kwenye makaburi ya jumla.

Serikali ya Congo imetangaza leo jumatatu siku ya kitaifa ya maombolezo. Mvua kubwa pia imenyesha hivi karibuni nchini Uganda na Kenya.

XS
SM
MD
LG